Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya |
Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika eneo la tukio na kusaidia majeruhi wa ajali hiyo. |
Huu ndio uskani wa basi hilo ni mbovu kupindukia na si salama kwa kutumika kwenye magari ya usafirishaji wa binadamu |
Kufuatia
kutokea kwa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mabasi ya
kampuni ya A.M,wananchi mkoani Tabora wameiomba Serikali kuyapiga
marufuku mabasi ya kampuni hiyo kwakuwa yamebainika kuwa ni mabovu na si
salama kwa wasafiri na wapita njia.
Wananchi hao
ambao walifika katika moja ya tukio la ajali iliyotokea eneo la Ipuli
mnadani kushuhudia ambapo wanafunzi wawili waliokuwa wakienda shuleni
kwa ajili ya masomo kwa muda wa ziada,mwanafunzi mmoja alifariki papo
hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na basi la A.M
Coach lenye nambari za usajili T 861 ATZ lililokuwa likifanya safari
zake kutoka Mwanza kwenda Tabora.
Aidha wananchi
hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamedai kuwa mabasi ya kampuni
hiyo yamekuwa yakiingia mjini kwa kasi kubwa huku yakionekana kuyumba
barabarani na kuzidi kutia shaka hata watumiaji wa barabara kuu za mkoa
wa Tabora.
Wameitahadharisha
Serikali kuwa endapo watayaachia mabasi hayo huenda yatasababisha ajali
mbaya zaidi na hata vifo visivyo vya lazima.
via>>kapipij blog
Post a Comment