Afisa
mmoja wa polisi mwanamke nchini Kenya amepewa onyo kali kwa kuvalia
sketi iliyokuwa imembana kiasi cha kuonyesha umbo lake.
Wakuu
wake walichukua hatua ya kumuonya polisi huyo baada ya picha yake
kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kupigiwa gumzo kubwa.
Alipigwa
picha akiwa amevalia sketi yake fupi na yenye kumbana akiwa anashika
doria katika eneo ambako mashindano ya magari yalikuwa yanafanyika eneo
la Kati mwa Kenya.
Afisa
huyo kwa jina Linda Okello, alitakiwa kufika mbele ya mkuu wake James
Mugeria na kuonywa vikali dhidi ya kuvalia hivyo kwa mara nyingine,
kitendo ambacho alifahamishwa kuwa ni utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo
isiyo ya heshima kwa polisi.
Maafisa
mjini Kiambu walisema kuwa kupewa onyo kwa afisa Linda na kuonywa dhidi
ya kuvalia sketi yake iliyokuwa imembana sana ni jambo la kawaida na
kwamba ameruhusiwa kuendelea na majukumu yake.
Waliongeza kuwa afisa huyo ameamrishwa kuanza kuvalia kiheshima.
Alipigwa
picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na
wenzake kazini mjini Kiambu. Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza
kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa
ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi
wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana.
via>>bbc
on Wednesday, April 30, 2014
Post a Comment