Wakazi
wa Kiwangwa, wa Kiwangwa, wakivushwa na vijana waliojitolea kujipatia
ajila katika Daraja la Ruvu kwa kuwavusha wananchi kwa kuwabea ama
kuwaongoza njia ili kuvuka eneo hilo la daraja lililojaa maji kutokana
na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Kamera ya Sufianimafoto
iliwashuhudia viajana hao wakiwavuja raia katika eneo hilo kwa ujila wa
Sh. 2000 kwa kila aliyebebwa mgongoni asiyetaka kuvua viatu ama kugusa
maji hayo, na Sh. 500 kwa kushikwa mkono kuongozwa njia kutoka mwanzo wa
maji hayo hadi kuyavuka, na kuyaongoza magari kuvuka eneo hilo ni Sh.
3000 hadi 5000.
Kutokana
na mvua kubwa iliyonyesha jana, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed
Kipozi, alifika eneo hilo na kujionea wananchi wakitaabika kuvuka ene
hilo na huku magari ya abiria yaliyokuwa yakitokea Bagamoyo kwenda
Kiwangwa, yakibeba abiria na kuishia eneo hilo na kubeba wengine
walioshushwa upande wa pili na kugeuza kwa kila abiria kulipa Sh. 1000.
Na kisha abiria hao wakipata usafiri mwingine wa kubebwa na Vijana
waliopo eneo hilo kwa Sh. 2000 kwa aliyependa ama 500 kwa kuongozwa
njia.
Vijana
hao wakiliongoza moja ya gari lililokuwa likivuka eneo hilo ambapo
dereva anafuata njia wanayopita vijana hao wa kulia na kushoto hadi
kuvuka ili kuoepuka kupita eneo hatarishi na kutumbukia ama kusukumwa na
maji hayo yaliyokuwa yakionekana kuwa na nguvu kubwa.
Mkuu
wa Wilaya ya bagamoyo, Ahmed Kipozi, akizungumza na watendaji wake
aliowaagiza kusimamia zoezi la kuwazuia wananchi kuvuka eneo hilo,
ambapo watendaji hao walimueleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wananchi
wamekuwa wakaidi na kuamua kukataa kutii amri na kuvuka, jambo
lililomfanya Mkuu wa wilaya kuamua kuagiza askari Polisi wenye silaha
ili kulinda eneo hilo kuwazuia waanchi kuvuka ili kuepuka maafa.
''WA HUKU WA HUKU NA WA HUKO WA HUKO''
Baada
ya hapo Mkuu huyo wa Wilaya aliwatoa tamko na kuwataka wakazi wa
Kiwangwa kutokwenda Bagamoyo na waBagamoyo kutokwenda Kiwangwa, kwa
kipindi chote cha mvua ili kuepuka maafa yanayoweza kutokea kwa
kutumbukia na kusombwa na maji, ama daraja hilo la Jeshi kukatika
kutokana na maji kuanza kupita juu ya daraja hilo jana.
Mkuu
wa Wilaya, akizungumza na madereva wa magari waliokuwa wakisubiri
kuvuka eneo hilo pamoja na vijana waliokuwa wakitoa huduma ya kuwavusha
watu.
Vijana wakifanya kazi yao ya kuwavusha watu eneo hilo.
Baadhi ya magari yaliyokaidi amri yakivuka eneo hilo.
Vijana
hao waliwavusha hadi wagonjwa katika eneo hilo kama anavyoonekana
pichani akiwa amembeba mtu mzima anayeonekana kuwa ni mgonjwa.
Baadhi ya vijana walijiona kama wapo Beach, walikuwa wakipiga mbizi na kuogelea eneo hilo kwa furaha.
Magari yakiwa katika foleni kusubiri kuvuka eneo hilo.
Baadhi
ya abiria walioshushwa upande wa pili wakiwania usafiri wa kuelekea
Bagamoyo baada ya kufaulishwa na gari jingine la uapnde wa pili.
Hawa nao ni wa upande wa pili
Gari la Abbas Tarimba likivuka eneo hilo.
Vijana wakijipigia debe kwa dereva ili akibali kuvushwa, bila kujua kuwa ndani yake alikuwapo Mkuu wa Wilaya hiyo.
Katapila lililoletwa ili kuziba eneo hilo kuzuia magari kuvuka....
Haya ni baadhi ya madaraja ya barabara mpya inayojengwa yakiwa yamejaa maji.
Dereva wa pikipiki akipakia gunia la mkaa vizuri ili awapakie na abiria wake wawili baada ya kuvuka darajani hapo.
Haya ni baadhi ya maeneo hayo yaliyojaa maji, ambapo mmoja wa vijana hao anaonekana akipiga mbizi kwa furaha.
'Bonge' la Mgahawa likiwa limejaa maji
Pembeni (kulia) ni mtumbwi unaotumiwa na wakazi wa eneo hili kuvuka kuelekea upande wa pili.
Imecotwa: mafoto blo
Post a Comment