Serikali
imeagiza gazeti la Mawio kueleza sababu za kupotosha na kukejeli nia
njema ya serikali kwa wananchi wake kuhusu Hati ya Muungano.
Akizungumza
jana, Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema
gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.
Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi Aprili 23, mwaka huu, kukanusha taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23,
mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Hati za Muungano utata’, taarifa
husika inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na
batili.
Linadai waandishi wawili ndiyo
waliona kati ya waandishi zaidi ya 20 waliokuwepo kwenye mkutano wa
Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
"Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazo na imeandikwa pasipo shaka kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua,” alisema.
Alisema pamoja na maelezo ya
Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua kwa utashi wake kukejeli na
kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya Muungano ina utata.
Post a Comment