PAZIA VPL LAFUNGWA, AZAM KUKABIDHIWA KOMBE CHAMAZI
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inafikia
tamati kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku
mabingwa wapya Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar
es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi
zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo Yanga na Simba
zitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mechi ambayo viingilio vyake
ni sh. 7,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya
chungwa, sh. 20,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tayari
tiketi zimeanza kuuzwa leo (Aprili 18 mwaka huu) katika vituo saba vya;
Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kariakoo (Kidongo Chekundu),
Buguruni Shell, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Ubungo
OilCom, Dar Live Mbagala na Uwanja wa Taifa.
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United (Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro), Rhino Rangers na Ruvu Shooting (Uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Mgambo Shooting (Uwanja wa
Sokoine, Mbeya), Oljoro JKT na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Sheikh Kaluta
Amri Abeid, Arusha) na Coastal Union na Kagera Sugar (Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga).
MICHUANO YA BEACH SOCCER KUANZA JUMAPILI
Michuano
ya mpira wa miguu ya ufukweni (Beach Soccer) inazinduliwa rasmi
keshokutwa (Aprili 20 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo
Mikocheni, Dar es Salaam na kushirikisha timu 13.
Uzinduzi
huo utaanza saa 5 asubuhi na mechi zitachezwa hadi saa 11 jioni.
Michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini inashirikisha timu
13 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.
Vyuo
hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (AU), Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania
(SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Chuo cha Ustawi
wa Jamii (ISW), Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) na Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Vingine
ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Utawala wa
Kodi (ITA) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Michuano
hiyo itakuwa inachezwa Jumamosi na Jumapili kwenye fukwe za Escape One
na Gorilla Beach iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.
WAZOEFU TAIFA STARS KUTAJWA KESHO
Wachezaji
wazoefu wa Taifa Stars watakaoungana na wale 16 waliopatikana katika
mpango wa maboresho wa timu hiyo watatangazwa kesho (Aprili 19 mwaka
huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itapiga kambi kwenye
hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya
Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Wachezaji
waliopatikana katika mpango wa maboresho ya Stars wanatarajiwa kuwasili
leo (Aprili 18 mwaka huu), na kwenda moja kwa moja kambini kuwasubiri
wenzao watakaotajwa kesho (Aprili 19 mwaka huu).
Wachezaji
hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Mara), Emma Namwondo Simwanda
(Temeke), Joram Nason Mgeveje (Iringa), Omari Ally Kindamba (Temeke),
Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala),
Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke) na Said Juma Ally (Mjini Magharibi).
Wengine
ni Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona
(Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara), Chunga Said Zito (Manyara),
Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala),
Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi) na Paul Michael Bundara
(Ilala).
Post a Comment