Hofu
imezidi kutanda miongoni mwa jamii hasa kundi la vikongwe baada ya
vikongwe wanne kuuawa kikatili kwa kukatwa mapanga wilayani
Geita,matukio hayo yakihusishwa na imani za kishirikina na migogoro ya
urithi wa ng’ombe na mashamba katika kipindi cha wiki moja.
Matukio
hayo yametokea siku chache baada ya mkuu wa wilaya,Manzie Mangochie
kutoa kauli mwishoni mwa wiki iliyopita ya kuwachukulia hatua za
kisheria viongozi wa maeneo yatakapotokea mauaji ya vikongwe.
‘’Tunayo
matatizo ya mauaji ya vikongwe,hali hii ni Aibu na hakuna mwenye
mamlaka ya kuondoa uhai wa binadamu,kuua mtu wa Mungu?,nendeni kuanzia
sasa mkaimarishe ulinzi kwenye maeneo yenu likitokea tukio tutawakamata
viongozi wa eneo husika’’alisema dc kwenye kikao cha madiwani.
Kamanda
wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo,akithibitisha jana(leo) kutokea kwa
matukio hayo alisema tukio la kwanza lilitokea Aprili 23,mwaka huu saa 2
usiku katika kijiji cha Katoma baada ya watu wasiojulikana kufika
nyumbani kwa Kulwa Kapalata(67)kuomba maji kabla ya kumshambulia kwa
kumkata kwa mapanga kikongwe huyo na kusababisha kifo chake.
Aidha
Konyo alisema Aprili 27,mwaka huu vikongwe watatu waliuawa kwa nyakati
tofauti katika vijiji vya Kagu,Butundwe na Kasamwa wilayani hapa kwa
kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.
Aliwataja
Waliouawa kwamba ni,Joyce Dotto(70)mkazi wa Butundwe ambaye aliuawa na
watu wasiojulikana akiwa eneo la shule ya msingi Chikobe akiwa njiani
kurudi nyumbani akitokea kwenye Klabu ya pombe za kienyeji.
Mwingine
ni Yombo Petrol(50)Mkazi wa Kanyala Kasamwa,akiwa nyumbani alivamiwa
nyumbani kwake saa 1 usiku na watu watatu waliomshambulia kwa mapanga
sehemu za shingoni na mikono na kusababisha kifo chake kisha wauaji
walichukua ng’ombe wawili wakaondoka nao.
Hata hivyo ng'ombe hao walikutwa hatua chache kutoka nyumbani kwa kikongwe huyo wakiwa wamekatwa miguu yote na wauaji hao.
Katika
tukio la tatu kikongwe mwingine aliyeuawa ni Kabula Yohana(60)mkazi wa
kitongoji cha Nchankungu kijiji cha Kagu,ambaye aliuawa kikatili kwa
kukatwa mapanga na kundi la watu wasiojulikana idadi yao na mara baada
ya kufanya mauaji hayo waliotoweka kusiko julikana.
Katika
kipindi cha mwaka jana vikongwe 15 waliuawa kikatili mkoani Geita kwa
imani za kishirikina na migogoro ya urithi wa mashamba na mifugo katika
wilaya za Geita,Chato na Bukombe.
Kufuatia
mauaji hayo baadhi ya vikongwe wanaishi kwa hofu kwenye familia zao
kutokana na kutuhumiwa kuhusika katika vifo vya baadhi ya ndugu,majirani
na jamaa zao baada ya kwenda kupigiwa ramli kwa waganga wa kienyeji
kutaka kujua waliohusika na vifo vya ndugu zao.
via>>geitayetu
Post a Comment