Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA YAWAFUKUZA KAZI WATUMISHI WALIOTOROKA KAZINI


 
Na Bongo leaks
HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa imewafukuza kazi watumishi wake sita, kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo utovu wa nidhamu na utoro kazini.
Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo, baada ya watumishi hao kwa nyakati tofauti kupewa onyo na kalipio kali.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Steven Mhapa alisema katika kipindi chote cha utovu wa nidhamu watumishi hao waliendelea kupokea mishahara yao kama kawaida.

“Ofisi ya Mkurugenzi ilileta rasmi ombi la kuwafukuza kazi watumishi hawa, hivyo baraza la madiwani limebariki kwani, hata sisi hatupo tayari kuona kazi zinalala kwa sababu za uvivu,” alisema
 
Aliwataja watumishi hao kuwa ni Andrew Mtavangu na Uswege Mwakosya waliokuwa Maafisa Elimu Wasaidizi Daraja la Tatu na Prosper Mzena aliyekuwa Mwalimu.
 
Wengine ni Sabath Masembo aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la Pili, Abdukadh Mnyavanu aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji na Godfrey Msuya aliyekuwa Tabibu Msaidizi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top