
Dar es salaam ndio mji unaoongoza kwa foleni ya magari Tanzania ambapo wakati mwingine unaweza kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu mpaka anaesafiri kwa ndege ya Fastjet kutoka Dar mpaka Zambia (dakika 135) au Kilimanjaro mpaka Dar es salaam (dakika
60) akawahi kufika kabla yako.
Unaambiwa
kati ya mwaka 2008 mpaka 2013 kuna jumla ya magari madogo laki mbili na
elfu ishirini na sita (226,806) yaliingizwa nchini Tanzania ambapo
asilimi 70 yanatumika Dar es salaam.
Kingine
cha kufahamu ni kwamba kwa mwezi, Watanzania hununua magari madogo
yanayokadiriwa kuwa zaidi ya 4500 ambapo mengi kati ya hayo hutumika
ndani ya jiji la Dar es salaam kwa mujibu wa @BBC_Habanahaba
Magari mengi yanayotumiwa ni kutoka kampuni ya Toyota Japan kama vile Mark X na aina nyingine mbalimbali huku Japan ikiwa ni nchi ambayo magari inayotengeneza yamekua yakipata soko kubwa sana kwenye nchi mbalimbali za Afrika kutokana na kuweza kuhimili mazingira magumu ya nchi zenyewe.
on Sunday, April 13, 2014


Post a Comment