Watu
10 wamenusurika kufa maji katika ziwa Victoria baada ya meli ya mizigo
Fb Matara kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari tani 280
zilizonunuliwa katika kiwanda cha sukari Kagera wakati ikitoka Bukoba
kwenda jijini Mwanza.
Meli
hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Mkombozi fishing and marine transport
limited, imezama ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani 280, mali
ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza aitwaye V.h. Shah, ambapo mkurugenzi
wa kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza kwamba meli hiyo imezama
ikiwa katikati ya visiwa vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku
na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo.
ITV
imeshuhudia meli hiyo ikiwa imepinduka huku juhudi za wafanyakazi wa
kampuni hiyo kuipundua zikiwa zinaendelea bila mafanikio, huku baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hiyo kuzama ni
kutokana na dhoruba kali ambapo wametoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo
vya majini kuzingatia utabiri unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa
nchini ili kuepusha maafa.
Meli
hii inayoonekana pichani ni mfano wa meli iliyozama,ambayo ilianza
safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa
na kapteni Erick Lasana – mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na
nchi kavu Sumatra kanda ya ziwa, umethibitisha kuzama kwa meli hiyo
yenye uwezo wa kubeba tani 280 za mizigo na abiria 100.
CHANZO: ITV TANZANIA



Post a Comment