Jeshi
la Polisi Tanzania limetangaza zawadi ya Tsh.Milion 10 kwa mtu
atakayewezesha kupatikana kwa wahusika walioshiriki mlipuko wa bomu
lililolipuka Arusha,Bomu hilo lililipuka mwishoni mwa wiki iliyopita
kwenye bar ya Arusha Night Park ambalo lilisababisha majeruhi kadhaa.
Mkurugenzi
wa makosa ya jinai Tanzania Dci Isaya Mgula amesema uchunguzi wa awali
uliofanywa na wataalam wa mabomu kutoka Jwtz na Jeshi la Polisi Tanzania
umebaini bomu hilo limetengenezwa kienyeji mbali na hilo lililolipuka
Jeshi la Polisi pia lilibaini bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba
uliokua umeeegeshwa pembeni ya kiti kwenye bar jirani ya Washington.
Post a Comment