Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KANISA LA WADVENTISTA WA SABATO MBEYA YATOA MSAADA KWA WAFUNGWA GEREZA LA RUANDA MBEYA






Waumini wa kanisa la Wadventista wa Sabato Jimbo la Nyanda za juu kusini  mkoani Mbeya limetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa wafungwa wa gereza la Ruanda jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Askofu Joseph Mngwabi, Mkurugenzi wa Afya na Mawasiliano Jimbo la Nyanda za juu kusini wa Kanisa la Sabato, Mchungaji Haruni Kikiwa, amesema ni sehemu ya kutimiza neno la Mungu.

Amesema msaada huo umetolewa na kanisa pamoja na waumini waishio ndani na nje ya nchi ambao wametoa zawadi mbali mbali ambazo zitanufaisha Gereza zima zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 3.7.

Amezitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na vyakula na matunda vyenye thamani ya shilingi Milioni 2,027,000 Nguo shilingi 240,000 na  vitabu vya dini 525 vyenye thamani ya shilingi million 1.3 ambavyo vilikabidhiwa gerezani hapo na kufuatiwa na ibada ya kawaida.

Kwa upande wake Mchungaji Eliot Kiswaga ambaye ni mkufunzi wa dini Gerezani hapo amesema ni vema taasisi zingine za kidini na mashirika binafsi yakajitoa kwa ajili watu wenye mahitaji kama wafungwa kwa kutoa misaada mbali mbali ili kuwatambua kama jamii ya kawaida.

Naye muumini wa Kanisa hilo, Tully Musyani, amesema kama waumini wa Kanisa la Wadventista wa sabato wanaguswa sana na binadamu wenzao wanaotumikia vifungo magerezani hivyo njia ya kuwafariji katika shida hizo ni kutoa misaada ya hali na mali.

Amesema kanisa kupitia kwa waumini wao na marafiki wanaoishi nje na ndani ya Nchi wameitikia wito wa kutoa vitu mbali mbali ili kuwafariji wafungwa gerezani pamoja na kutoa pongezi kwa Wahitimu wa mafunzo ya neno la Mungu yaliyotolewa na Chuo cha Sauti ya unabii chenye makao makuu mkoani Morogoro.

Mafunzo hayo yamewanufaisha Wafungwa 262 na Askari 20 wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Ruanda mkoani Mbeya wamehitimu mafunzo ya Biblia yaliyotolewa na Chuo cha sauti ya unabii kinachomilikiwa na Kanisa la Wadventista wa Sabato nchini.

Mwisho.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top