Kiongozi
wa Kikundi cha Kataa Unene Family (KUF) ambaye pia ni mwandishi na
mtangazaji wa Televison ya Taifa (TBC1), Angella Msangi amekemea tabia
ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia picha zao ili waweze kuuza
biashara zao za madawa ya kupunguza uzito.
Akizungumza
na Kajunason Blog kwa masikitiko makubwa, Kiongozi huyo alisema kuwa
kuna wafanyabiasha ambao si waaminifu wamekuwa wakichukua picha zao
katika mitandao ya jamii na sehemu nyingine na kutangazia biashara zao
kuwa hao wametumia dawa zao na wamepungua.
Pichani
ni Kiongozi wa Kikundi cha Kataa Unene Family (KUF) ambaye pia ni
mwandishi na mtangazaj wa Televison ya Taifa (TBC1), Angella Msangi
akiwatambulisha wanakikundi wenzake mbele ya Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph Mwenda. Hii ilifanyika mwishoni mwa mwaka jana mara
baada ya kushiriki Mbio za Uhuru. (Picha na Maktaba.)
“Kiukweli
nimechukizwa na tabia hii ambayo kwa sasa imesambaa kwa wafanyabiasha
wengi wa madawa ya kupunguza uzito, wanachukua picha zetu na kusema
wametuuzia dawa zao na tumepunguza uzito… Naomba watambue kuwa sisi
tunafanya mazoezi na ulaji bora (diet) ndiyo maana tunapungua uzito”,
alisema Angella.
Aliongeza
kuwa kwa sasa wameshawasiliana na mwanasheria wao na watawafikisha
mbele ya sheria watu wote ambao si waaminifu wanataka kujipatia kipato
kwa njia ya udanganyifu wa picha za watu.
Wanakikundi
wa KUF wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni na
Michezo, Fenella Mkangala. Hii ilifanyika mwishoni mwa mwaka jana mara
baada ya kushiriki Mbio za Uhuru. (Picha na Maktaba.)
Hili
ni moja ya tangazo lililotumiwa na wafanyabiashara hao kuonyesha jinsi
bidhaa zao zinavyopunguza unene wakati si kweli, huyu ni mmoja ya
wanachama wa KUF.
Kundi la KUF linawanachama
wapatao 50 ambao hukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja huku
wakihamasishana kila muda kufanya mazoezi na kujitahidi kula vyakula
vitakavyojenga mwili.
Post a Comment