
Rais Uhuru Kenyatta
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imehairisha kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hadi tarehe saba Oktoba mwaka huu.
Rais
Kenyatta anatuhumiwa kwa makosa ya jinai kufuatia machafuko ya baada ya
uchaguzi wa mkwaka 2007 - 2008, madai ambayo ameyakanusha.
Mahakama
kuu ya ICC, kupitia mwendesha mashitaka Fatou Bensouda, imekuwa
ikiitaka serikali ya Kenya kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuendesha
kesi zinazowakabili Rais Kenyatta na naibu wake bwana Ruto.
Hii ni mojawapo ya sababu kuu ya kubadili tarehe ya kusikizwa kwa kesi hii.
Upande
wa mashitaka umesema kuwa unaipa Kenya muda wa ziada ili kutafuta na
kuwasilisha baadhi ya stakabadhi za benki zinazohitajika katika kesi
hiyo.
Kumekuwa
na malalamishi kutoka kwa upande wa mashitaka kuwa serikali ya Kenya
inalenga kuzuia stakabadhi hizo kufikishwa mahakamani jambo ambalo
mawakili wa bwana Kenyatta wamekanusha.
Miongoni mwa yale yanayohitajika kotini ni pamoja na taarifa ya maelezo ya fedha anazomiliki bwana Kenyatta.
Kesi
hii imekumbwa na matatizo ya mashahidi kujiondoa na shutuma za mahakama
hii kuonea viongozi wa bara Afrika.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment