WIZARA ya Mali Asili na Utalii kwa kushirikiana na wadau
wengine hapa nchini wamefanikiwa kuendesha doria ambayo iliweza
kufanikisha kupungua kwa kasi ya ujangili hapa nchini kwa asilimia 58
tofauti na mwaka jana ambapo ujangili ulikuwepo kwa kiwango cha juu sana
Aidha doria hiyo ya Mandays pia iliweza kufanikisha kukamatwa
kwa mali gahafi ambazo zilikuwa zkitumika na majangili hayo ambayo
yamekuwa yakisababisha madhara makubwa sana kwa taifa la tanzania Akiongea
na vyombo vya habari mapema leo Mkurugenzi wa idara ya wanyama pori
taifa Paulo Sarakikya alidai kuwa oparesheni hiyo ilianza rasmi toka
januarya hadi kufikia mwezi machi mwaka huu na takwimu zinaonesha
mafanikio makubwa sana kwani doria hiyo pia iliweza kuhusisha ujangili
wa ndani na hata ule wa nje ya hifadhi.
Aliendelea kwa kusema kuwa katika kipindi husika jumla ya
mizoga ya tembo 39 ilionekana ndani na nje ya hifadhi za taifa na mapori
ya akibanchini huku meno mazima yakiwa ni 171 na vipande 22 vya meno ya
tembo ghafi , vipande 302 vya meno ya tembo yaliyochakatwa yenye jumla
ya kilo 662.62 pamoja na nyama pori zenye jumla ya kilo 1,111 ambazo
nazo zilikuwa ni kwa ajili ya vitoweo vya majagili hayo.
Sarakikya alidai kuwa mbali na kukamata vitu hivyo pia waliweza kukamata vitu vingine kama vile
Bunduki ya rashasha moja, Rifle 3, shotgun 2, gobori 5 na
jumla ya risasi 7 za aina mbalimbali pamoja na malighafi kama vile
magari 5 ngombe 2663 misumeno 1 na mbao 745
kutokana na hilo pia watuhumiwa
waliweza kulipa faini ya zaidi ya milioni 25 na pia hali hiyo iliweza
kusababisha hata ujangili kushuka kwa kiwango cha asilimia 58 tofauti na
mwaka jana ambapo ujangili ulikuwa ni mkubwa sana.
NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA
on Tuesday, April 1, 2014
Post a Comment