mali zilizoteketea kwa moto
|
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao Huu kuwa moto huo chanzo chake kimesababishwa na mtoto mdogo ambae
alikuwa ndani ya nyumba hiyo akichezea moto ndani ya nyumba hiyo
na kusababisha moto huo kushika makochi yaliyokuwemo ndani ya
nyumba hiyo.
Nyumba
hiyo mali ya Bi Grace Mpewa imenusurika kuteketea yote baada ya
wananchi wa eneo hilo kuendelea kuzima moto huo bila ya kutoa
taarifa jeshi la zima moto na uokoaji mjini hapa kiasi cha moto huo
kuteketeza sehemu kubwa ya nyumba hiyo .
Balozi
wa eneo hilo la Zizi la Ng'ombe Edmundi Kikula alisema kuwa
baada ya kuzuka moto huo walifika kutoa msaada na kuanza kuzima
moto huo huku mmiliki wa nyumba hiyo bila kuwepo na kuwa mtoto
huyo baada ya kuulizwa alidai kuwa mama yake ndie aliacha jiko la
moto huo .
Alisema
kuwa mali mbali mbali zimeteketea kwa moto huo huku baadhi ya
vitu vikiokolewa na kuwa walishindwa kutoa taarifa kwa wakati
zimamoto kutokana na kukosa namba zao .
Hata
hivyo aliwataka wananchi wenzake kuhifadhi namba za Zimamoto ili
kutoa taarifa kwa wakati pindi majanga kama hayo yanapojitokeza
badala ya kuelekeza lawama kwa kikosi hicho.
Kwa
upande wake stafu Sajenti wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mjini
Iringa ambae alikuwepo eneo la tukio Bw Juma Joseph Mkuvalo
alisema kuwa kufika kwao eneo hilo ni baada ya kuitwa na jeshi la
polisi kufuatia mtandao huu kufikisha taarifa
za tukio hilo.
Mkuvalo
alisema jamii inapaswa kukabiliana na matukio ya moto pale
yanapojitokeza na kuwa huduma hiyo haina malipo yoyote na kuwataka
wananchi kutumia namba za zimamoto ambayo ni 114 ili kutoa taarifa.
kwa hisani ya wa www.matukiodaima.com
bbbbbbbb
Post a Comment