Katibu wa chama cha mapinduzi CCM W/ Ya
Mufindi Miraj Mtaturu akiwa na mjumbe wa halmashauri kuu CCM - MNEC
Wilaya ya Mufindi ambaye pia ni mwenyekiti wa UWT W ya Mufindi
Marcellina Mkini, katika hafla ya kuwapokea viongozi hao waliohama
CHADEMA.
Zawadi Waziri Shombe aliyekuwa mjumbe wa Oparesheni
ya M4C kanda ya kusini, akizungumzia azma ya yeye kujiunga na CCM.
Bernado Lugenge aliyekuwa katibu mwenezi CHADEMA, akitoa neno la ushuhuda mara baada ya kujiunga na CCM.
Aliyekuwa Katibu wa Chadema Jimbo la Mufindi Kusini - Emanuel Ngwalanje, akishuhudia jambo, katika hafla hiyo.
Wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka CHADEMA wakila kiapo cha utii.
VIONGOZI wa chama cha demokrasia na
maendeleo CHADEMA nyanda za juu kusini, wamekihama chama hicho na kujiunga na
chama cha mapinduzi CCM kwa madai kuwa wamechoshwa na ubabaishaji.
Viongozi
hao waliohama CHADEMA ni
pamoja na Katibu wa Chadema) Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel
Ngwalanje, alikuwa katibu wa CHADEMA jimbo la Mufindi Kusini, Zawadi
Waziri Shombe ambaye alikuwa ni mjumbe wa Oparesheni ya M4C Nyanda za
juu kusini, pamoja na Bernado Lugenge aliyekuwa Katibu Chadema.
Wamesema hatua hiyo ya kujitoa Chadema na kujiunga CCM ni kutokana na hali isiyoeleweka juu ya chama hicho na hivyo kuamua kujiunga na CCM ili kuungana na wananchi wenzao katika kuleta maendeleo.
Wamesema hatua hiyo ya kujitoa Chadema na kujiunga CCM ni kutokana na hali isiyoeleweka juu ya chama hicho na hivyo kuamua kujiunga na CCM ili kuungana na wananchi wenzao katika kuleta maendeleo.
Ngwalanje amesema katika kipindi cha
zaidi ya miaka minne alichokuwa Katibu wa Chadema Jimbo la Mufindi Kusini
ameweza kushawishi zaidi ya wakazi 600 katika maeneo mbalimbali jimboni humo ambao
waliweza kujiunga na chama hicho.
Naye Zawadi
Shombe aliyekuwa mjumbe wa oparesheni ya M4C kanda ya kusini amesema demokrasia
inayohubiriwa kutafutwa na chadema nchini ina walakini kwa kuzingatia kwamba
ndani ya chama hicho zipo nafasi za uongozi ambazo wanachama wengine wamekuwa
hawapatiwi fulsa ya kuzimiliki.
“Nimeamua kurudi nyumbani, nyumbani kwa baba
yangu na mama yangu CCM, ili nishirikiane na wana Mufindi wenzangu kuleta
maendeleo ya Taifa,” nimetumika vya
kutosha Chadema na hakuna nilichofanya cha muhimu, zaidi ya upotoshaji na
vurugu tupu,” Alisema.
Aidha
Bernado Lugenge aliyekuwa katibu mwenezi CHADEMA tawi la Kimilinzowo,
amesema hatua ya wao kuingia CCM ni pigo kubwa kwa Chadema kwani wao
ndiyo walikuwa mstari wa mbele kutete na kushawishi, ili kukifanya
chadema kuwa imara Mufindi.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamesema CHADEMA imepata pigo kufuatia viongozi hao kuondoka kwani walikuwa ni nguzo kuu wilayani Mufindi.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamesema CHADEMA imepata pigo kufuatia viongozi hao kuondoka kwani walikuwa ni nguzo kuu wilayani Mufindi.
“Hawa watu walikuwa wanaushawishi
mkubwa sana CHADEMA, na walikuwa wanaogopewa
na wana CCM, walikuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi na kujenga hoja na hali
hiyo ndiyo imewavuta wananchi wengi kujiunga na chamdema,” Walisema.
Hatua ya viongozi hao wa chadema
kurudi CCM imepokewa kwa furaha na wana CCM huku wananchi wa kijiji cha Kimilinzowo
wakipata manufaa kupitia tukio hilo kwani furaha ya viongozi waliohudhuria
hafla hiyo imewafanya watoe ahadi ya kusaidia mifuko zaidi ya 50 ya Saruji kwa
ajili ya ujenzi mbalimbali uliokuwa umekwama.
Baada ya kukabidhi kadi na magwanda
ya Chadema kwa uongozi wa CCM wilaya ya Mufindi na baadaye kupewa mavazi na
kadi ya CCM, Ngwalanje na wenzie wamesema kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuisambaratisha
Chadema katika wilaya hiyo ya Mufindi na mkoa mzima wa Iringa.
“Kazi ya kuibomoa Chadema sasa
imeanza, na kazi hii haitaishia katika wilaya ya Mufindi tu, tutaiendeleza hadi
Jimbo la Iringa Mjini ambalo linaloongozwa na mbunge Mchungaji Peter Msigwa
kupitia Chadema.” Walisema.
Marcelina
Mkini mjumbe wa
Halmashauri kuu CCM Taifa "MNEC" na mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT
Wilaya ya Mufindi amesema tukio hilo la kipekee linapaswa liwe Baraka
kwa kuwapa
ushirikiano vijana hao, pasipo kuwabagua.
“Vijana hawa wanatosha jamani, tumewasikia
walivyojieleza hapa na namna walivyokuwa ni nguzo huko nChadema, kwa kweli kwa
hili niwapongeze sana ndugu zangu kwa jambo hili tunalolishuhudia leo, kwani ni
jambo linaloonyesha kuwa tupo imara, kwani tungewaacha vijana hawa waendelee
kuyumbayumba tungeonekana hatutoshi ndani ya chama chetu, tunatakiwa tuwape
ushirikiano wa kutosha, kwani hata makanishani wanaorudi kundini hawapaswi
kunyoshewa kidole, kwani hali hii ni ishara ya kudumisha amani katika chama
chetu, ” Alisema mkini.
Aidha Mkini amesema katika Wilaya ya
Mufindi hakuna wanawake waliojiunga na Chadema kwani wanafahamu kuwa kunapotokea
machafuko na kukosekana amani wanaopata taabu ni akinamama na watoto, na kuwa
suala hilo ambalo ni ishara ya amani linapaswa kuendelezwa zaidi kwani ni jambo
la kujivunia.
Katibu wa CCM Wilay ya Mufindi Miraji
Mtaturu, amesema ushuhuda huo ni Baraka hata mbele ya Mwenyezi Mungu, kwakuwa aliweka utaratibu
wa kuwasamehe watu wanaotubu dhambi zao.
Mtaturu amesema katika siasa watu
wanaoamua kumaliza tofauti na kurejea katika chama tawala ni sawa na mwana
mpotevu anaporudi nyumbani, anatakiwa kusamehewa dhambi na kufanyiwa sherehe ya
kumpongeza kwa ujasiri, huku akiwapongeza vijana hao kwa ujasiri wa kutambua
umuhimu wa wao kuwa ndani ya chama chenye kuwaletea wananchi maendeleo.
"Ninawaombeni wanaCCM wenzangu tushirikiane na vijana wetu hawa, kwa hali na mali, kwani wao wenyewe wamepima na kuona CCM ndiyo chama imara, niwaombeni kusiwepo na ubaguzi wa aina yoyote juu yao, ni vijana wanaofanya kazi za uimarishaji wa cha, nadhani mnawafahamu ni wenzenu, amani, upendo ndiyo msingi wa kila kitu kuyafikia maendeleo," alisema Mtaturu
"Ninawaombeni wanaCCM wenzangu tushirikiane na vijana wetu hawa, kwa hali na mali, kwani wao wenyewe wamepima na kuona CCM ndiyo chama imara, niwaombeni kusiwepo na ubaguzi wa aina yoyote juu yao, ni vijana wanaofanya kazi za uimarishaji wa cha, nadhani mnawafahamu ni wenzenu, amani, upendo ndiyo msingi wa kila kitu kuyafikia maendeleo," alisema Mtaturu
Amesema CCM ina furaha kubwa
kuendelea kuwapokea watanzania waliopotea kwa kujiunga na vyama vya upinzani na
baadaye kubaini makosa waliyoyafanya na kuamua kurudi katika chama
kinachohimiza amani, utulivu kwa lengo la kuboresha maisha ya raia wake na
kuwaletea maendeleo wananchi.
Na Oliver Motto
Post a Comment