Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Lindi Mjini na Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini mtoto Idd Omar kutoka
katika Kijiji cha Madangwa , kata ya Sudi huko Lindi Vijijini. Mama
Salma alifika kijijini hapo kwa ajili ya kupokea mbio za uzalendo za
pikipiki zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana, (UVCCM) kitaifa zikitokea
Mkoa wa Mtwara tarehe 17.4.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya
Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara
kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya
zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa
ya kuambukizwa. Baadhi
ya wasichana na akina mama wakionyesha umahiri wao katika kucheza ngoma
za utamaduni wakati wa sherehe ya makabidhiano ya mbio za pikipiki
kutoka mkoani Mtwara kwenda Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa
tarehe 17.4.2014.Mwenyekiti
wa CCM wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Said Sinani (mwenye kofia)
akifuatana na viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Vijana
kwenda kukabidhi mbio za pikipiki kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi kwenye
Kijiji cha Madangwa tarehe 17.4.2014.
Mwenyekiti
wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani akikabidhi picha ya Baba
wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ali
Mtopa na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman
Karume kwa Mama Salma Kikwete kuashiria muendelezo wa mbio za uzalendo
za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar
hapo tarehe 26.4.2014.Mjumbe
wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa
Kijiji cha Madangwa na wageni waliohudhuria sherehe ya kupokea mbio za
pikipiki kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Mtwara na
Lindi katika kusherehekea miaka 50 ya Mungano.Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwahutubia
wananchi wa Kata ya Mingoyo wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki
kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele tarehe 26.4.2014.Viongozi
wa juu wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana mbio za pikipiki
kusherehekea miaka 50 ya Mungano.Bwana
Salum Musa Mtungulu mkazi wa Kijiji cha Madangwa alitumia fursa hiyo ya
makabidhiano ya mbio za pikipiki kurejea Chama Cha Mapinduzi akitokea
Chama Cha NCCR- Mageuzi. Katika picha hiyo anatoa maelezo ya kitendo
hicho huku makada wakimvisha mavazi ya Chama Cha Mapinduzi.Mjumbe
wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana
na wananchi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja kilichoko katika Kata ya Mingoyo
walifurika kushuhudia sherehe za mbio za pikipiki za uzalendo
kusherehekea miaka 50 ya Mungano .Baadhi
ya wasichana na akina mama wakionyesha umahiri wao katika kucheza ngoma
za utamaduni wakati wa sherehe ya makabidhiano ya mbio za pikipiki
kutoka mkoani Mtwara kwenda Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa
tarehe 17.4.2014.Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama
Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3,
aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama
mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha
Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo tarehe
18.4.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Post a Comment