Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea maelezo
kutoka kwa Afisa wa Bunge Bwana Patson Sobha, wakati alipowasili kwenye
Banda la Bunge la maonesho ya maadhisho ya miaka 50 ya Muungano wa
Tanzania yanayoendelea katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Maonesho hayo yatakayofikia kilele siku ya Jumamosi Aprili 19, ikiwa ni
maandalizi ya siku kuu ya Muungano ambayo huherekewa Aprili 26 kila
mwaka.
Rais
Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya vitabu na
nyaraka mbalimbali za Bunge na Bi. Devotha George alipotembelea banda la
Ofisi ya Bunge kwenye Maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano
katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
on Friday, April 18, 2014
Post a Comment