Ronaldo |
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo ana matumaini ya kurejea Jumanne dhidi ya Bayern Munich katika
mechi yao ya kwanza ya nusu fainali. "Nina furaha sana. Nilitaka kucheza
na kuisaidia timu (dhidi ya Barcelona) lakini wachezaji wenzangu
walifanya kazi nzuri. Nazidi kuwa fiti sasa, sisikii maumivu yoyote.
Huenda nikarejea dhidi ya Bayern au katika mechi ya marudiano nao."
Mwanasoka Bora huyo wa FIFA, alikosa
michezo kadhaa ikiwamo wa Fainali ya Kombe la Mfalme wakati Real Madrid
ikiizamisha Barcelona kwa kuifunga mabao 2-1, huku yeye akiwa jukwaani
kabla ya kujumuika pamoja klushangilia taji hilo.
Post a Comment