Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO KWA WANAFUNZI WA KIKE WA VYUO VIKUU NA SEKONDARI HUKO DODOMA

IMG_7576IMG_0370Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kupokewa na Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rehema Nchimbi tarehe 11.4.2014.
IMG_0421 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwa shamrashamra za kwaya na matarumbeta wakati alipotua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.

IMG_0467Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipanda mti eneo la jengo la utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya kufungua rasmi kongamano la Mustakabali wa mtoto wa kike katika mazingira ya sasa kwa wanafunzi  wa kike wa vyuo vikuu vilivyopo Dodoma na Morogoro. Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Chimwaga  tarehe 12.4.2014.IMG_0500 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa ukumbini na wanafunzi wa kike waliojawa na furaha na hamasa kubwa.
IMG_0524Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza kwa nderemo na vifijo na wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu mbalimbali vya Dodoma na Morogoro wimbo uitwao  ..”wanawake na maendeleo..” mara baada kuingia ukumbini. Mama Salma alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kongamano la mustakabali wa mtoto wa kike katika mazingira ya sasa.
IMG_0589Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma  Profesa  Herman Mlacha akimkabidhi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete zawadi ya ramani ya Tanzania yenye kuonyesha pia picha ya Chuo Kikuu cha Dodoma  mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo tarehe 12.4.2014.IMG_7576 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wanafunzi  wa kike kutoka vyuo vikuu waliofurika katika ukumbi wa Chimwaga huko Dodoma tarehe 12.4.2014.
IMG_0549
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top