Katibu
Mtendaji wa UNCTAD Dkt Mukhisa Kituyi (Kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya
Mtangamano wa Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw Lucas
Saronga( Katikati) na Balozi wa Uswizi nchini Olivier Chave(Kulia)
wakisaini hati za makubaliano ya utekelezaji mradi wa SECO.
Picha
ya pamoja ya wafadhili na wawakilishi wa Serikali ya Tanzania
walioshiriki uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika Jijini Arusha.
Picha ya pamoja ya Washiriki wote wa Mkutano na uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika mjini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika Jijini Arusha.
Mradi
wa kuunganisha sekta za Wazalishaji matunda, mbogamboga na wenye hoteli
(SECO) unaofadhiliwa na Serikali ya Switzerland umezinduliwa Jijini
Arusha.
Mradi
huo ambao lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya watanzania
wanaojihusisha na sekta hizo kwa kuongeza uzalishaji wao na uhakika wa
masoko ya ndani na nje ya nchi, unaanza utekelezaji wake mara moja ukiwa
na thamani ya jumla ya Dola za Ki marekani milioni tatu na nusu.
Uzinduzi
wa Mradi huo umeshuhudiwa na Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt Mukhisa
Kituyi, Balozi wa Uswizi nchini Tanzania Bw Olivier Chave na Mkurugenzi
wa Idara ya Mtangamano wa Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara
Bw Lucas Saronga.







Post a Comment