Na Hudugu Ng'amilo.

Jaji
Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana
amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza
maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya
Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba.
Akizungumza
kwa ukali, Jaji Warioba alisema: "Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga
muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?
"Sheria
inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano
usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna
ya kuboresha Muungano."
Katika
swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la
Muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa
Serikali ya Muungano ya sasa siyo ya Muungano, ni ya Tanganyika.
Katika
swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi
ambao waliieleza tume hiyo kuwa Katiba imevunjwa na madaraka ya rais
yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.
"Tume
inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani
kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia
sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba
katika swali lake la nne.
Katika
swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za
kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikali tatu kwa sababu yeye
pamoja na (Joseph Butiku) walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na
Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu
ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.
Pia,
aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki
kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake wanageuza
rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika
swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume
ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya
maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
Alisema
badala ya kujadili hoja za msingi, wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa
wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu (akiwamo na yeye),
kitendo ambacho alisema si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu
yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi.
Katika
uzinduzi huo walikuwepo baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ambao ni Dk
Hamisi Kigwangalla aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, Julius Mtatiro, Maria Sarungi na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole.
Amshukia Lukuvi.
Katika
maelezo yake, Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwake na wajumbe
kulitumia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kama mfano wa kuwashawishi
Watanzania kukubaliana na matakwa yao ya kutaka kupinga mfumo wa
serikali tatu.
"Nchi hii
imekuwa na matatizo ya rushwa na ufisadi, lakini hakuna hata siku moja
mtu amesema jeshi linaweza kushika madaraka. Leo kwa sababu ya madaraka
mnaingiza jeshi na mchakato wa Katiba katika makundi."
Licha ya
kutomtaja mlengwa, kauli hiyo ilionekana kumlenga Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi ambaye Aprili 13,
mwaka huu aliwataka wananchi kupinga muundo wa serikali tatu, akisema
la sivyo jeshi linaweza kuchukua madaraka.
Akiwa
katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa mgeni rasmi
akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Lukuvi alisema muundo huo
ukipita, nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano
itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.
Kauli kama hiyo pia iliwahi kutolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
"Msiliingize
jeshi katika siasa za makundi na inakuwa mbaya zaidi kama mkienda
katika makanisa na kutoa kauli za namna hii," alisema Warioba na
kuongeza:
"Umoja
wetu, amani na utulivu kwa kiwango kikubwa mhimili wake ni viongozi wa
dini. Wamekuwa wakihubiri umoja, amani na mshikamano, hivyo tusiingize
siasa za makundi kwenye makanisa na misikiti."
Jaji
Warioba aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kukumbuka wajibu wao wa
kuwaunganisha wananchi na kuwataka waachane na kauli za kejeli, kuudhi
na matusi kwani zinaweza kuleta mgawanyiko na mpasuko nchini.
"Nimekuwa
mtumishi wa umma kwa muda mrefu lakini sijawahi kuona taasisi yenye
uzalendo wa hali ya juu kama JWTZ," alisema Warioba.
Warioba
ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania,
kuanzia mwaka 1985 hadi 1990, alisema: "Katika ziara zangu mikoani
nilikuwa nikikutana na wanajeshi na kunieleza matatizo yao. Licha ya
wakati huo serikali za mataifa mengine zilikuwa zikipinduliwa na jeshi,
hapa kwetu ilikuwa tofauti, walikuwa na uzalendo wa hali ya juu licha ya
kuwa hali yetu kiuchumi ilikuwa mbaya," alisema.
Alisema
wakati huo wanajeshi walikuwa wakivaa sare zilizochakaa na viatu
vilivyopasuka, lakini hawakufikiria kuipindua Serikali.Alisema hata
katika vita dhidi ya Uganda, wanajeshi wa Tanzania walishinda kwa sababu
ya uzalendo na siyo vifaa vya kisasa vya kivita... "Inashangaza kuona
watu wanatolea mfano mmoja tu wa kama wanajeshi wasipolipwa; kwa nini
wasiseme mawaziri au watumishi wa serikali wasipolipwa?"
Alisema
kauli hiyo ni sawa na kuwaeleza wananchi kuwa jeshi ni baya na kama
ikipita Katiba isiyoendana na matakwa ya walio wengi jeshi litachukua
nchi.
Alisema
wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikikusanya maoni ya wananchi,
wanajeshi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini walijikita
zaidi kutoa maoni ya kuimarishwa kwa ulinzi na usalama na siyo mambo
mengine.
"Tatizo
ambalo walitueleza ni kuchoshwa na kitendo cha kupiga mizinga 21 kwa
Amri Jeshi Mkuu wakiwa Dar es Salaam na wakiwa Zanzibar. Walisema kwa
nidhamu ya jeshi, Amri Jeshi Mkuu ni mmoja tu. Nadhani mngewaondolea
kero hiyo na si mambo mengine," alisisitiza.
Kigwangalla.
Kwa
upande wake, Dk Kigwangalla alisema kama tatizo ni Muungano ni vyema
suala hilo likarejeshwa upya kwa wananchi ili watoe maoni yao kwa sababu
mchakato huo sasa umehamia katika muundo wa Muungano pekee.
"Mchakato
huu si wa kuifufua Tanganyika na kuvunja mkataba wa Muungano na siyo wa
kubadili muundo wa utawala. Mambo haya yalihitaji mchakato
unaojitegemea," alisema.
Alisema
tume zote zilizotoa mapendekezo ya Serikali tatu zilikuwa na asilimia
ndogo ya watu waliounga mkono kama ilivyo kwa Tume ya Jaji Warioba.
CHANZO MWANANCHI.
Post a Comment