Kamati ya Mazishi ya Mzee Muhidin Maalim Gurumo ikiwa imekaa kujadiliana maswala mbali mbali.
Mjane
wa Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) juu ya maisha yake na Marehemu mumewe.
Wadau wa Muziki.
Mpiga Solo wa Bendi ya Msondo,Ridhiwan Pangamawe akiwa ni mwenye majonzi kwa kuondokewa na Kiongozi wake.
Mzee King Kikii na wadau.
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta,Asha Baraka akiambatana na wanamuziki wake wakiwasili msibani hapo.
Wakisabahiana.
Mzee
King Kikii,Rashid Pembe na Abdul Salvador wakiwajadiliana mambo kadha wa
kadha juu na namna walivyomkumbuka Mzee Muhidin Maalim Gurumo.
Sehemu
ya Waombolezaji wa Msiba wa nguli wa Muziki wa Dansi hapa nchini na
aliekuwa kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Marehemu Mzee Muhidin Maalim
Gurumo wakiwa nyumbani kwake Mabibo (Tabata Makuburi),leo.Shughuli zote
za Mazishi zinaendelea nyumbani hapo.Tarati bu za Mazishi
zimefanyika,yatafanyika kesho Aprili 15,2014 kwenye Makaburi yaliopo
kwenye kijiji cha Masaki,Kisarawe mkoani Pwania.
Mmoja
wa wanamuziki wa zamani na aliewahi kufanya kazi Pamoja na Marehemu
Mzee Muhidin Maalim Gurumo,Mzee Shaaban Dede (wa pili kushoto) akiwa ni
miongoni mwa waombolezaji waliofika kwenye msiba huo.
Sehemu ya Waombolezaji wakiwa msibani hapo.













Post a Comment