NI
gumzo la aina yake ndani ya mji wa Kibaha mkoani Pwani ambapo mume wa
mtu aliyejulikana kwa jina la Vedasto Ager (43) mefariki dunia baada ya
kupata ajali ya kugongwa na gari aina ya Fuso akiwa amempakiza mke wa
mtu kwenye pikipiki.
Kifo cha Vedasto kilichotokea Aprili 6, mwaka huu kimeacha maswali kibao kutokana na muda
Mwanamke
huyo alijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu
wa chanzo kimoja, marehemu Vedasto alikuwa akifanya kazi ya kuuza
tiketi kwenye mabasi yaendayo mikoani huku mwanamke huyo akifanya kazi
ya kuuza chakula ambayo ni maarifu kwa jina la Mama Lishe.
Uwazi lilifika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao walisema
hakuna anayejua kuwa wawili hao walikuwa wakitokea wapi kwani wote
walikuwa mbali na maeneo wanayoishi! “Hata sisi tunashangaamarehemu
alikuwa amembeba mke wa mtu saa saba usiku
wakitokea wapi kwenda wapi?” alihoji mkazi mmoja.
Uwazi
lilipata bahati ya kuzungumza na mume wa majeruhi huyo, Fautunatus
Simon ambapo alisema: “Mimi nilikuwa napita, ghafla niliona ajali.
Nilipokwenda pale nilikuta kila mtu ameanguka kivyake. Nilipowaangalia
vizuri nikagundua mmoja ni mke wangu akiwa na Vedasto. “Vedasto
alifariki dunia palepale lakini mke wangu alikuwa ana majeraha, hatua ya
kwanza niliwakimbiza Hospitali ya Tumbi nikishirikiana na
wananchiwengine.
Waombolezaji.
Vedasto
aliingizwa mochwari lakini mke wangu alipelekwa Muhimbili.”
Akizungumzia tuhuma za marehemu kuwa na uhusiano na mke wake, mume huyo
alisema hata yeye amezisikia na akasema atamuuliza mkewe akipata nafuu.
“Binafsi marehemu nilikuwa namfahamu sana lakini sijapata ukweli kuwa
usiku ule walikuwa wanatokea wapi?” alisema.
Kamanda wa Polisi tukio hilo. “Gari lililosababisha ajali hiyo halijapatikana lakini polisi wanaendelea na upelelezi,” alisema.
-GPL


Post a Comment