OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers inaendelea! Wiki hii ilifanya kazi nyingine nzito, kumnasa Pastor John Paul Simon Rubanguka
wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar ambaye
alinaswa akichezewa utupu na wanawake watatu ambao ni kama waumini wake
kwa sababu wote ni Wakristo.
Pasta
John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance
lililopo Masaki, Dar baada ya kunaswa na wanawake watatu wakimchezea
utupu.
OFM YATONYWA UCHAFU WA PASTOR
Ilikuwa Jumanne ya Aprili Mosi, 2014, saa
4:14 asubuhi, chanzo cha habari kilipiga simu chumba cha habari cha
Global na kuwataka makachero wa OFM ambapo alipounganishwa nao alisema:
“Jamani kama kweli hapo ni OFM nina
malalamiko. Mimi nimeshtukia mchezo mchafu unaotaka kufanywa na pastor
(mchungaji) mmoja anaitwa Rubanguka.
Pasta John Paul Simon Rubanguka akijaribu kujitetea.
“Huyu pastor
amempa dili dada mmoja kumtafutia wasichana wazuri watatu na kuwapeleka
kwenye nyumba moja hivi kisha wawe wanamchezea utupu wake huku wao
wakiwa kama walivyozaliwa, ndiyo furaha yake ilipo. Wasichana
wameshapatikana.”
MSHIKO WA NGUVU NA SAFARI JUU
Mtoa habari huyo aliendelea kudai kuwa,
pastor huyo alisema wasichana watakaokuwa wakichezea utupu atawafanyia
usaili wa kwenda kuwauza kwenye kasino moja iliyopo Uarabuni ambayo yeye
ni wakala wa kuwapelekea malaya huko.
Pastor akiwa na mmoja wa wanawake waliofumaniwa naye.
Chanzo hicho
kiliendelea kudai kuwa, pastor huyo aliwaahidi wanawake hao kitita cha
shilingi 300,000 kila mmoja kwa wale watakaofaulu kumchezea vizuri,
sanjari na kuwakatia hati za kusafiria ‘passport’.
Makamanda wa OFM wakimtuliza Pasta.
OFM YAWEKA MTEGO
Baada ya kupata ishu nzima, OFM ilifanya
ukachero na
kugundua mahali ambapo tukio hilo lilipangwa kufanyika, ni
kwenye danguro moja lililopo Kinondoni jijini Dar.
Wanawake walionaswa katika tukio hilo wakivaa viwalo vyao.
OFM ilifika
kwenye nyumba hiyo na kufanya ushushushu wake ambapo walifanikiwa kuweka
mitambo yao sambamba na kulishirikisha jeshi la polisi kwa ajili ya
kumnasa mtumishi huyo wa Mungu akifanya vitendo hivyo.
Saa 8:11
mchana, OFM wakiwa wamejibanza eneo hilo waliwashuhudia warembo watatu,
weupe wakielekea kwenye nyumba ambayo mtoa habari wetu aliielekeza.
Kitambulisho cha Pasta.
PASTOR AWASILI KWA MBWEMBWE
Saa 11:23 jioni, OFM wakiwa hawajaanza
hata kujisikia kuchoka, walimwona pastor huyo akiwasili kwa mbwembwe
akiwa ndani ya gari dogo na kugeuza kwa staili ya kupiga ‘norinda’ kisha
akashuka. Mkononi alishika maji makubwa. Alipokelewa na mmoja wa
wanawake hao.
Bango lililopo Kinondoni Mkwajuni, Dar likieleza lilipo kanisa la Pasta huyo.
MCHEZO WAANZA
Saa 11:40 jioni, makachero wa OFM
walifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa, tayari mchezo ulishaanza
ambapo waliwataarifu polisi na kuungana nao kwenda kuvamia nyumba hiyo.
Msafara wa OFM na polisi hao ulifika nje
ya chumba kilichokuwa kikidaiwa kufanyika uchafu huo. Sauti ya muziki
na wanawake waliokuwa kama wapo kwenye darasa la siri zilisikika.
Polisi waligonga mlango na kujitambulisha kisha wakaomba wafunguliwe mlango haraka ndani ya sekunde chache.
PASTOR APATA MCHECHETO
Pasta John na wanawake hao walitii amri
kwa kufungua mlango ambapo mchungaji huyo alikumbwa na mchecheto na
kutaka kurukia juu ya dari lakini polisi walimtafadhalisha kutulia
pamoja na wanawake hao kama walivyo.
OFM ikiwa chumbani humo iliwashuhudia wanawake hao wakiwa watupu mbele ya pastor huyo ambapo walikuwa wakimnengulia viuno.
Baada ya kupewa kibano, warembo hao
walimwanika pastor huyo kwamba ndiye aliyewatuma wamchezee wakiwa watupu
ili awalipe shilingi laki tatu kila mmoja, pia kuwapeleka Uarabuni
kwenye kasino.
UTETEZI WA PASTOR
Kwa upande wake, Pastor John alijitetea
kuwa anaomba asamehewe kwa gharama zozote ili taarifa hizo zisifike
popote kwani ishu hiyo ilikuwa si amri yake bali shetani alimpitia.
“Jamani naomba tumalize humuhumu ndani,
mnajua mimi ni Pastor wa Kanisa la Maximum Deliverance, sasa ukweli ni
kwamba waumini wangu hawatanielewa, chondechonde ilindieni kazi yangu
jamani,” alijitetea.
Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio,
pastor huyo na wanawake ‘wake’ walikuwa kwenye harakati za kupelekwa
mbele ya vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zinazostahili.
KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI
Siku zote kazi ya OFM ni kuwajibikia
matendo maovu na si kuwaonea watu kwa lengo la kuwachafua. OFM
inapopata habari huichunguza ukweli wake kwanza kabla ya kuchukua hatua
ya kuifanyia kazi moja kwa moja, yaani kufika kwenye eneo la tukio.
Lengo kubwa la kutoa habari za aina hii
ni kuwakumbusha watu namna ya kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Wengi wamebadilika, sasa wanaishi vizuri wakiwa watu wapya na
wanyenyekevu pia wenye kufundisha wenzao
Post a Comment