Mkurugenzi
wa Sera, Mpango na Utafiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi
Tanzania (TACAIDS) Dkt. Raphael Kalinga akiwaeleza jambo waandishi wa
Habari( Hawapo pichani) Wakati wa Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa
Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar Es Salaam.Kushoto ni Afisa
Habari Mkuu wa Tume Hiyo Bi. Nadhifa Omar.
…………………………………………………………………………………….
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Tume
ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imedhamiria kuanzisha
Mfuko wa Ukimwi utakaolenga kuondoa upungufu wa Rasilimali katika maeneo
mbalimbali ili kuboresha afua za ukimwi nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sera, Mpango na Utafiti wa Tume hiyo Dkt. Raphael Kalinga leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Kalinga alisema kuwa uanzishwaji wa Mfuko huo ni moja yakipaumbele
kilichowekwa na Tume hiyo katika kuimarisha uratibu wa utekelezaji wa
mkakati wa taifa wa kudhibiti Ukimwi kwa mwaka wa Fedha 2014/2015.
“Katika
kuendelea kuimarisha uratibu wa utekelezaji wa mkakati wa taifa wa
kudhibiti Ukimwi kwa mwaka wa Fedha 2014/2015 Tume imeamua kuweka
vipaumbele ikiwamo kuanzisha mfuko wa UKIMWI( ATF) utakaolenga kuondoa
upungufu wa Rasilimali katika maeneo mbalimbali ili kuboresha afua za
ukimwi nchini” Alisema Dkt. Kalinga.
Aidha
Dkt. Kalinga aliongeza kuwa mfuko huo unategemewa kuaza ifikapo Julai,
2015 na kuanza jukumu la kuhamasisha utafutaji wa Rasilimali za
kudhibiti Ukimwi Nchini.
Pia
Dkt. Kalinga alibainisha kuwa Tume itaendelea kutoa kipaumbele cha afua
za Vijana hasa walio katika umri kati ya miaka 15 hadi 24 waliopo
shuleni na nje ya shule kwa kuwa ndio kundi lenye changamoto ya rika
balehe na pia ufahamu mdogo ambao ni sawa na asilimia 40.3 kwa wanawake
na 47.3 kwa wanaume kwenye masuala ya ukimwi.
Pia
Dkt. Kalinga aliongeza kuwa kundi hilo halina hamasa hasa katika
masuala ya upimaji wa Ukimwi na Matumizi ya kinga, baadhi wanajihusisha
na tabia hatarishi ikiwamo kujiunga na makundi hatarishi, wanachangia
kwa asilimia kubwa maambukizi ya ukimwi kulingana na utafiti wa
viashiria vya ukimwi na malaria wa Mwaka 2011/2012.
TACAIDS imepanga kuhamasisha Halmashauri zote nchini kutenga fedha za udhibiti UKIMWI kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya Ndani.
Post a Comment