Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula akifungua mkutano wa wadau
mkoani Geita unatakaojadili mchakato wa uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya
Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA).
Katibu Tawala wa Mkoa Severine Kahitwa akieleza umuhimu wa kuwa na utaratibu wa TIKA ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.
Wadau wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo.
………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Geita
MKUU
wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula amezindua rasmi mchakato wa
uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi
(TIKA) huku akiwataka wadau kuhakikisha wanapitisha mpango huo kwa
maslahi ya wananchi wa mkoa huo.
Magalula
ameyasema hayo wakati akizindua mpango huo kwa wadau mbalimbali kutoka
Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo amesisitiza kuwa bila ya wananchi
kujiunga katika utaratibu wa TIKA itakuwa ni vigumu kumudu gharama za
matibabu ambazo zinaongezeka kila kukicha.
“Jamani
wenzetu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wametuletea mpango huu ni
vyema tukaujadili kwa makini na kwa mtazamo chanya ili hatimaye
Halmashauri ya Mji ianze utekelezaji wa suala hili…utaratibu wa
kuchangia kabla ya kuugua ni mzuri na unakupa uhakika wa kupata huduma
za matibabu wakati wowote,” alisema Mkuu wa Mkoa.
Alisema
kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiingia kwenye matatizo mbalimbali
yakiwemo ya madeni ama kuuza vitu vya nyumbani kwa ajili ya kupata fedha
za matibabu hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwa
familia husika hivyo akasisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa TIKA ili
kuondokana na matatizo hayo.
Hata
hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa hakusita kuutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
kuhakikisha unabadilika au kubadili mbinu zake za uhamasishaji kwa
kuwafuata wananchi ambao wako katika vikundi mbalimbali vya uzalishaji
mbinu ambayo itarahisisha kuwafikia wananchi wengi zaidi na uchangiaji
wake utakuwa ni rahisi tofauti na kumfuata mtu mmoja mmoja.
“Endeleeni
na uboreshaji wa huduma za matibabu na kuangalia ni namna gani
mtamaliza au kupunguza tatizo la ukosefu wa dawa katika vituo vya
kutolea huduma ili wananchi wasiwe na visingizio wakati wa kujiunga na
mipango kama hii,” alisema.
Aidha
aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuweka utaratibu mzuri
wa uwekaji wa kumbukumbu za wanachama kwa kuwa ndizo zinazotoa picha
halisi ya mahitaji yaliyopo ndani ya halmashauri ama mkoa kwa ujumla.
Akizungumzia
uboreshaji wa huduma za afya ndani ya Halmashauri hiyo, alimwagiza
Mganga Mkuu kutumia fursa zinazotolewa na NHIF za mikopo ya vifaa tiba
na ukarabati wa majengo kwa lengo la uboreshaji wa huduma za matibabu.
“Mbali
na fursa ya mikopo hii pia ni vyema matumizi ya fedha zitokanazo na
CHF/TIKA i zikatumika kwa kufuata miongozo iliyotolewa na Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii ambayo asilimia 67 itumike kwa kununulia dawa,
asilimia 15 itumike kwa uboreshaji wa huduma za afya na inayobaki ndo
inaweza kutumika kwa shughuli zingine ambazo zinahusiana na masuala ya
afya,” alisema.
Kwa
upande wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao uliwakilishwa na Meneja
wa CHF, Constantine Makalla alisema kuwa lengo la Mfuko ni kuhakikisha
kila halmashauri inaanzisha na kutoa huduma kwa kuwa na sheria ndogo
ambapo hadi Desema 31, 2013 jumla ya Halmashauri 128 zilikuwa na sheria
ndogo.
Alisema
kuwa mipango ya NHIF kwa mwaka huu ni kuongeza uwigo wa wanachama,
kuanza utaratibu wa kuzizawadia Halmashauri zinazofanya vizuri na
uboreshaji wa daftari la CHF/TIKA na taarifa za wanachama wake nchi
nzima.
Post a Comment