Mwalimu
 wa Shule ya Msingi Misunkumilo, Kata ya Namanyere, wilayani Nkasi, 
mkoani Rukwa, Oswald Kapota (33) amehukumiwa kwenda jela miezi sita kwa 
kosa la kutelekeza familia yake na kwenda kuishi kwa kimada.
Mwalimu
 huyo ambaye ameshindwa kubaki njia kuu na kuendeleza michepuko, amepata
 hukumu hiyo juzi baada ya Mahakama ya Mwanzo Namanyere, kumtia hatiani.
Akitoa
 hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Namanyere, Baraka Stanley, 
alisema kuwa mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande 
wa mashitaka ambao unaonyesha kuwa Mwalimu huyo alifanya kitendo hicho 
kwa kukusudia.
Mwalimu
 huyo alidaiwa kuitelekeza familia yake ya watoto wawili na mke, kisha 
kuhamia nyumbani kwa  mwanamke mwingine na kuifanya familia hiyo kuishi 
katika mazingira magumu kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, hali 
iliyomlazimu mkewe kufungua kesi polisi ya kudai huduma ya malezi ya 
familia hiyo.
 Licha
 ya hukumu hiyo mahakama imeamuru mwalimu huyo atakapomaliza adhabu yake
 ya kifungo jela atalazimika kuitunza familia yake kama wajibu 
unavyomtaka kama mzazi.
Awali
 upande wa mashitaka uliieleza mahakama hiyo kuwa mwalimu huyo 
alimtelekeza  mke wake, Lucy Malambugi, ambaye amezaa naye watoto wawili
 kiasi cha kuifanya iishi maisha magumu huku mkewe akihangaika kuomba 
omba ilhali yeye akiponda raha na nyumba ndogo.
Kabla
 ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshitakiwa alitakiwa kujitetea ambapo 
alikataa kutoa utetezi wake kwa madai kuwa hawezi kujitetea mbele ya 
mwanamke huyo, akimtuhumu kuwa  si mwaminifu kwenye ndoa na ndiyo chanzo
 cha yeye kuamua kuhamia kwa nyumba ndogo.
Kutokana
 na kosa hilo, mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo chini ya kifungu 
cha sheria namba 167, sura ya 16, ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 
2002.
Via>>Tanzania Daima

 


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Post a Comment