 MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, Khamis  Kigwangala, amemtuhumu 
Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta, kuliendesha kwa  upendeleo, 
uonevu na ushabiki.
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, Khamis  Kigwangala, amemtuhumu 
Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta, kuliendesha kwa  upendeleo, 
uonevu na ushabiki.
 Kigwangala alisema Sitta, amekuwa na tabia ya  kupendelea wachache 
huku akidai kufanya hivyo ni kutenda haki, jambo ambalo si  sahihi.
 Kigwangala alitoa tuhuma hizo jana asubuhi  alipotaka mwongozo wa 
Mwenyekiti juu ya muda wa dakika 16 alizopewa Msemaji wa  wachache, 
Tundu Lissu, kumalizia hotuba yake iliyokatishwa wiki iliyopita baada  
ya TBC kukatisha matangazo ya moja kwa moja.
 Kigwangala alisema Lissu, alikuwa amebakiza  dakika mbili, lakini 
alishangazwa na uamuzi wa Sitta kuwa mjumbe huyo amebakiza  dakika 16.
 “Mimi pia  niliambiwa wakati nasoma hoja ya kamati yangu, lakini TBC
 walikuwa wakikata  matangazo lakini nilipokuandikia kuhusu jambo hili 
hukunisikiliza, lakini kwa  Lissu naona unafanya hivyo, sasa unaona 
kuwapendelea wachache ndiyo kutenda  haki?” alihoji.
 Akijibu  mwongozo huo, Sitta alisema tuhuma hizo zimemsikitisha kwa 
kuwa mambo mengi  anayoyafanya anategemea wataalamu waliopo bungeni 
hapo.
 “Nasikitika kutuhumiwa nafanya upendeleo, mimi  nategemea wataalamu 
wao ndiyo wanashika saa na wao ndiyo wanasema umebaki muda  fulani, mimi
 sitazami saa yangu na kuamua.
 “Ikiwa  hawa watatu wamekosea basi ni bahati mbaya wao ndiyo 
wamesema hizo dakika 16 si  mimi, ni kweli jana Jumapili, uliniletea 
barua nyumbani kulalamikia kuhusu  kutopewa nafasi kama Lissu,” alisema.
 Sitta alisema baada ya kuipata barua ya  Kigwangala alimpa maelekezo
 Katibu wa Bunge afuatilie TBC, kujua kama lina  ukweli ndani yake na 
baadae ilithibitika kuwa wakati wa Kigwangala akiwasilisha  maoni 
hakukuwa na tatizo la kukatika kwa matangazo.
 “Jamani  hili la Lissu halikuwa langu, nilitahadharishwa na 
Mheshimiwa Freeman Mbowe,  wote tukafuatilia tukabaini ni kweli,   sasa 
hili la Kigwangala, halikutolewa tahadhari,” alisema.

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Post a Comment