MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiwa ni mkazi wa Dar leo asubuhi aligongwa na gari aina ya Toyota Coaster inayofanya shughuli za daladala kwenye barabara za Morogoro jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Urafiki jijini Dar es Salaam. Walioshuhudia tukio walisema majeruhi huyo alikuwa katikati ya barabara mbili akitaka kuvuka kuelekea eneo la kituo cha polisi cha Urafiki lakini bahati mbaya aliyumba na kudondokea daladala hiyo iliyokuwa nyuma yake ambayo ilimburuza kwenye ukingo wa barabara hiyo.Picha mbalimbali zikionesha Wasamaria wema wanavyomuokoa majeruhi huyo.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL
Post a Comment