Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kumbe Wanafunzi waliozama na meli korea kusini walituma msg kwa wazazi kabla.

 


Screen Shot 2014-04-17 at 4.07.50 PM
Meli ya Korea Kusini iliyokua imebeba zaidi ya abiria 460 wengi wakiwa ni Wanafunzi, ilizama kusini mwa pwani ya nchi hiyo siku ya Jumatano asubuhi ambapo mpaka sasa wengi hawajapatikana huko Korea Kusini ilikozama na ni siku moja tu baada ya ajali ripoti zimeanza kutoka za msg zilizotumwa na wale waliokuwa wamekwama ndani ya meli hiyo.

140417120950_ujumbe_wanafunzi_512x288_bbc_nocredit
          Msg ya mwanafunzi mmoja kwa mamake wakati meli ikizama.

Mwanafunzi:’huenda hii ndio mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,’ndio ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake.
Mama:”na mimi nakupenda mwanangu,” alijibu mama yake Shin kwa ujumbe wa simu bila kujua kilichokuwa kinaendelea.
Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kuwaona watoto wao.
Screen Shot 2014-04-17 at 4.07.24 PM
Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja na babake , yalinukuliwa na shirika la habari la AFP ni haya hapa chini
Mwanafunzi: “baba usijali,nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.”
Baba: Najua msaada uko njiani,lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.”
Mwanafunzi: ”Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama”
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.
Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafuzni mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli ilipoanza kuzama.
Mwanafunzi: “meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini’
Kakake:” usiwe na wasiwasi fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari.’ baada ya hapo hakukua na mawasiliano mengine yaliyoendelea.
melii
Stori imeandikwa na BBC.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top