Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa
katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za
abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio
Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.
BASI aina ya Coster linalofanya ruti zake
Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na
Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. ZAIDI ya
abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini
Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na
kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana
wa siku ya jana. Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo
maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo
imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa
mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi
breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari
matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa,
Tax pamoja na Hiace. Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo ,
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius
Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi
watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi
kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao
kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
Post a Comment