
Naibu Waziri wa Fedha(S) Mh:Mwigulu
Lameck Nchemba(Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Tanzania Bara ataongoza
Sherehe za Kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Kwa Watanzania
Waishio Nchini Marekani-Washington-DC na Viunga Vyake.
Maadhimisho hayo yanayotegemewa Kufanyika Tar.26/04/2014 katika Ukumbi wa MATINICE EVENTS AND CONFERENCE CENTRE,7925 CENTRAL AVE,CAPITOL HEIGHTS,MD 20743.
Mh:Mwigulu Nchemba aliyealikwa na Balozi
wa Tanzania Nchini Marekani Mh:Libereta Mulamula kuongoza Sherehe hizo
za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano,atazungumza na Watanzania kuhusu
Muungano Wetu,Kuulinda,Kuutetea na Kuudumisha kwa Manufaa ya Taifa letu
la Tanzania na Watu Wake.
Watanzania Wote Mnaombwa Kufika kwa
Wingi kwenye
Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhai wa Muungano Wetu,Hii ni nafasi nzuri kwa
Watanzania Nchini Marekani kuandika Historia Mpya kwa Taifa letu.
Mungu Ubariki Muungano Wa Tanzania,
Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Ofisi ya Naibu Waziri wa Fedha(S)
Mawasiliano.
23/04/2014
Post a Comment