Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

POLISI YAWASHAURI WAFANYABIASHARA ARUSHA

 

MNGULUDCIJeshi la polisi limewataka wafanyabaishara wakubwa hasa wamiliki wa kumbi za starehe,Jiji la Arusha na Halmashauri zake zote kuhakikisha kuwa wanaweka vifaa vya kujihami (CCTV CAMERA) ili kuweza kugundua wanaotaka kusababisha milipuko ya mabomu.
Aidha kauli hiyo inakuja siku moja mara baada ya watu wasiofahamika kutega bomu katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Arusha Night Park, huku bomu lingine tena likiwa limetegwa katika baa nyingine ijulikanayo kama Washington Baa mapema juzi
Hayo yameelezwa mjini hapa na Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai Isaya  Mngulu wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na Hali ya Arusha kukumbwa na milipuko ya mabomu ya mara kwa mara.
Alidai kuwa mpaka sasa takwimu zinajionesha kuwa tukio hilo linajirudiarudia sana na hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kuanzia sasa kwani hatamabomu ya kienyeji nayo yanatumika sana kuuua lakini pia kujerui watu

Alisema kuwa hata uongozi mzima wa mkoa wa Arusha nao unatakiwa kuhakikisha kuwa kuanzia sasa unaanza mikakati ya kufunga vifaa mbalimbali ambavyo vitakavyoweza kuwabaini wahalifu wote wa mabomu kwani uwezekano wa kuwatambua hata kupitia vifaa hivyo upo.
aliongeza kuwa wamiliki wa kumbi za starehee nao pia wachukue tahadhari kuanzia sasa ambapo wanatakiwa kulinda uhai wa wateja wao na kamwe wasijisahau ingawaje nao wanahitajika kuwa na vifaa vya kisasa hasa CCTV CAMERA ili kuharakisha zaidi upelelezi.
“kutokana na hali ya mabomu ilivyo kwa sasa ni muhimu sana kwa kila mtu kuweza kuchukua tahadhari ingawaje na sisi tutahakikisha  kuwa tunawalinda ipasavyo wananchi wetu na hatutaweza kuruhusu  tena Arusha ikapata na janga lingine la mabomu ingawaje pia tunaimarisha ulinzi kila kona hususani kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu”aliongeza Isaya 
Katika hatua nyingine alisema kuwa Jeshi la polisi Nchini limetangaza kitita cha Milioni 10 kwa mtu yeyote atakayewezesha kutoa taarifa sahihi na kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyesababisha mlipuko wa bomu katika nyumba ya kulala wageni (Arusha Night Park)
Alimalizia kwa kusema kuwa katika tukio hilo la kurushwa kwa bomu la kienyeji katika nyumba hiyo ya kulala wageni hali za majerui zinaendelea vizuri na kwa sasa majerui nane wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Arusha.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top