Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS KIKWETE NA WANAFUNZO KATIKA PANTONI, AHANI KIFO CHA KADA WA CCM, APOKEA TUZO ALIYOTUNUKIWA MAREKANI



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe wakiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la  awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na viongozi hao waliokuwa wakielekea kuhani msiba wa kada wa CCM Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasala awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na na baadaye kutelemka na Rais aliyekuwa akielekea kuhani msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika Kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa  heshima za mwisho kwa mwili wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakiangalia cheti cha heshima alichopewa na Gavana wa Maryland wakati wa kupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membekupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kupokea toka kwa  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membekupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.( Picha na Ikulu )
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top