


BAO
pekee la Karim Benzema katika dakika ya 19` limeipatia ushindi muhimu
Real Madrid katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo, klabu ya Bayern
Munich kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid nchini Hispania.
Bao
hilo limewapa nguvu Real Madrid na kuwaongezea morali kueleka katika
mchezo wa marudiano jumanne ya wiki ijayo katika dimba la Allianz Arena.
Kama Real Madirid watachuku kombe mwaka huu basi watakuwa wamechukua taji hilo mara 10.
Kocha
Carlo Ancelotti na timu yake wangepata mabao mengi katika mechi ya leo
na kuwa na uhakika wa kufika fainali ya UEFA tangu waliposhinda taji
hilo mwaka 2002.
Cristiano
Ronaldo na Angel di Maria walikosa nafasi nzuri za kufunga na sasa
wamejipa kazi ngumu Allianz Arena kwasababu Bayern Munich ni timu hatari
na haitataka kuvuliwa ubingwa kirahisi kwao.
Kikosi
cha Real Madrid: Casillas, Carvajal, Fabio Coentrao, Alonso, Pepe
(Varane 73), Ramos, Modric, Isco (Illarramendi 82), Benzema, Di Maria,
Ronaldo (Bale 74)
Kikosi
cha Bayern Munich: Neuer, Rafinha (Javi Martinez 66), Alaba, Kroos,
Boateng, Dante, Robben, Lahm, Mandzukic, Schweinsteiger (Muller 74),
Ribery (Gotze 72)
Mechi hiyo imechezeshwa na mwamuzi Howard Webb kutoka nchini Englan
Post a Comment