Mwenyekiti wa Umoja Asasi za Kiraia, Bw. Irenei Kiria akifafanua jambo
mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Tathimini
zilizofanywa na asasi za kiraia kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba
mpya unaoendelea katika Bunge la Katiba mjini Dodoma, Katika tahimini
yao hiyo, umoja huo umegundua madhaifu mengi sana ambayo kama
hayatapatia ufumbuzi wake basi katiba mpya yenye kumjali mtanzania ni
Ndoto kupatikana. Pembeni ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Bi Kijo Bisimba.
Baadhi ya Wanachama wa Asasi za Kiraia (AZAKI), wakifuatilia kwa makini.
Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko hilo.
Kila mmoja akifuatilia kwa karibu...
Tupenda kuipongeza serikali na hasa kumongeza kwa dhati Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kukubali kuansiha mchakato wa kutunga katiba mya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunalishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutunga
sheria zote zinazowezesha kuelekeza hatua mbali mbali za mchakato huu.
TUnaishukuru Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Uongozi wa Jaji
Joseph Sinde Warioba kwa kuendesha zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa
wananchi na kuandika rasimu ya kwanza nay a pili za Katiba Mpya.
Tunawashukuru wananchi, wataalamu na Asasi mbali mbali kwa kushiriki na
kutoa maoni katika hatua mbali mbali za mchakato huu wa kutunga Katia
Mpya.
Kutokana na namna mambo yananvyokwenda katika Bunge Maalum la kutunga
Katiba, Asasi za Kiraiaziliona umuhimu kukutana kuanzisha tarehe 8
Aprili 2014 kutafakari yanayojiri na kukubaliana utakuwa mchango wa
Asasi katika kuhakikisha Tanzania inapata katiba mpya inayokidhi
mahitaji ya sasa na ya vizazi vijavyo. Baada ya vikao vya mara kwa mara
na majadiliano mengi pamoja na kukusanya taarifa kadhaa. Hatimaye katka
kikao cha tarehe 15 Aprili 2014 tulikubaliana tamko.
Kwa hiyo sisi Asasi za Kiraia tumekubaliana ya kwamba:
Kwa kuwa huu ndiyo mchakato pekee hapa Tanzania wa kutunga katiba mpya
ambao umewahusisha wnanchi tangu hatua za awali, tunauunga mkono na
kuutakia mafanikio.
Kwa kuwa Rais wa Jamhuri wa Tanzania amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha
katiba mpya inapatikana kabla ya kipidi chake cha uongozi kuisha, ni
vema Bunge Maalum la Katiba likazingatia yafuatayo;
1. Sisi Asasi za Kiraia tunaunga mkono Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
kama ilivyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kwa kuwa imekidhi
mahitaji ya Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo kama ikipita
itaimarisha uadilifu, uwazi, uwajibikaji, amani na umoja wetu.
2. Kwamba hatujafurahishwa na mijadala ndani ya Bunge Maamul la Kutunga
Katiba mijadala ambayo imepoteza utaifa na badala yake imejikita kwenye
kutoheshimiana, ubabe, ubaguzi, vijembe na vitisho.
3. Kwamba tumehuzunishwa sana na tabia ya kudhihakiana na kudharau
Rasimy ya pili ya Katiba pmoja na tume ya mabadiliko ya katiba na hasa
Mwenyekiti wake.
4. Tunaona kwamba mwennendo wa mijadala ni kuelekea kutetea maslahi ya
watawala wa vyama vya siasa badala ya maslahi ya utaifa na ustawi wa
wananchi.
5. Kwamba kitendo cha baadhi ya wajumbe kupendekeza kutoa maneno;
uwajibikaji, uadilifu, uwazi katika kipengele cha tunu za taifa inatia
mashaka kama nia ya Bunge Maalum la Katiba ni kutuletea katiba
itakayotutatulia matatizo hayo.
6. Kwamba hatufurahishwi na malumbano yasiyo na tija yanayochukua muda
mrefu kwenye mambo madogo madogo. Hii inapelekea kupoteza muda na hivyo
kutumia rasilimali za umma vibaya.
7. Kwamba hatujafurahishwa na kufungwa kwa tovuti ya Tume ya Mabadiliko
ya Katiba. Na pia hakuna juhudi za serikali kuwafikishia wananchi Rasimu
ya Katiba mpya na kuwaelimisha maudhui yake.
8. Tumeelewana kwamba tulikosea kutuga sheria inayohusu wabunge wa
kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la katiba. Kwa kawaida
watatetea maslahi yao kwanza kabla ya maslahi ya wananchi. Mfano bunge
la Tanzania lina wabunge 357, lakini rasimu inapendekeza wabunge 75 tu.
Hili ni tishio la wazi kwa maisha ya kisiasa ya baadae ya wabunge
madalakani sasa na hivyo wanapata umoja wa kupambana kuhakikisha rasimu
hii isipate ka ilivyo.
9. Tunaelewa pia kwamba, Rasimu hii imependekezwa kupunguza madaraka ya
Rais ya kuteua viongozi na watendaji wa serikali. Jambo hili, kwa
mtazamo wetu ni tishio kwa wagombea urais kwamba hawatakuwa na nguvu ya
kuahidi wapambe wao nafasi za uteuzi ili wawaunge mkono kwenye kampeni
ya uchaguzi.
Rai yetu Umoja wa AZAKI.
Tunasihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Uongozi wa Bunge hilo kurekebisha hizo kasoro walizozieleza.
Irenei Kiria
Mwenyekiti wa Umoja wa Asasi za Kiraia (AZAKI).
Post a Comment