Uongozi na
Wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Uingereza (UNITED KINGDOM) pamoja
Watanzania wanaoishi nchini Uingereza kwa pamoja wanajumuika na Watanzania wote
katika Kuadhimisha kilele cha sherehe za miaka hamsini (50) ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar zitazofanyika Tarehe 26 Aprili, 2014
katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, na pia kuwaombea
shamrashamra za amani na Utulivu katika Mkesha wa Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar utakaofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Tanzania Bara na Viwanja vya
Maisara, Zanzibar kuanzia saa 4:00 usiku wa tarehe 25 April 2014.
Vile vile Mwenyekiti wa CCM UK anayemaliza muda wake Ndugu
Maina A Owino anapenda kutoa shukrani za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. JAKAYA KIKWETE
kwa kuonyesha weledi mkubwa katika kuulinda na kuutetea Muungano wetu
wenye manufaa makubwa kwa Watanzania toka pande zote mbili.
Chama cha Mapinduzi Uingereza, Viongozi, wanachama wote na watanzania kwa ujumla hapa
UK wanasisitiza Kanuni za Msingi za
Muungano wa mwaka 1964 zinaonyesha dhahiri chimbuko la Muungano , pamoja na
mambo mengine linajumuisha uhusiano wa karibu wa muda mrefu kati ya watu wa
Tanganyika na Zanzibar, uhusiano wa kisiasa uliotokana na harakati za kupigania
uhuru zinazofanana na imani ya pamoja ya Uhuru wa Afrika yote. Ni Muungano
pekee unaodumu Leo hii kwenye Bara la Afrika kwa kuwezekana kuunganga kwa
mataifa mawili huru yanayojitawala. Tukio hili limeonyesha kwamba kuwa na
dhamira ya dhati na kuwa na ari na moyo kwa watu wa Afrika na viongozi wao,
inawezekana kuwa na umoja wa Afrika. Imedhihirika kuwa muungano kati ya
Tanganyika na Zanzibar ndiyo umoja pekee ambao bado unaendelea kudumu na kuwa
ni wa kipekee sana na wenye kuleta hamasa ya nchi mbali mbali duniani kote kutaka kujifunza kutoka katika Muungano wetu.
Kitendo cha
Waasisi wetu kukubaliana na kubadilishana Kanuni zenye misingi ya Muungano ndiyo nguzo kuu ambayo Taifa letu
linapasa kuilinda na kujivunia pamoja na
changamoto mbalimbali zinazotukabili, kuchanganya udongo wa Tanganyika na ule
wa kutoka Zanzibar inaonyesha ni kiasi undugu wetu ulivyo wa karibu na wenye
mahusiano ya damu moja ya KITANZANIA.
Katika kipindi
hiki cha mchakato wa Katiba Watanzania tusikubali kugawika kutokana na
propaganda za kisiasa na watu wachache zenye kujenga chuki miongoni mwetu
katika pande hizi mbili za Muungano.
Muungano ni wa
kwetu na wala siyo wa wanasiasa au makundi machache yenye dhamira na malengo
yao binafsi; hivyo tunawaomba Watanzania wenzetu tujikite katika kutoa michango
na mawazo yenye mashiko yatakayoboresha zaidi Muungano wetu wenye manufaa mengi
miongoni mwetu toka pande zote mbili.
TUDUMISHE MUUNGANO
WETU WA KIPEKEE DUNIANI
MUNGU IBARIKI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Imetolewa na
Abraham Sangiwa – Idara ya Itikadi, Siasa na Uenezi
CHAMA CHA
MAPINDUZI TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM
Tarehe 24/04/2014.
Post a Comment