Mkutano wa kumi na mbili wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaaanza rasmi hii leo mjini Arusha nchini Tanzania.
Miongoni mwa maswala muhimu yatakayojadiliwa ombi la Sudan Kusini kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.Mkutano wa mwisho kama huu uliofanyika mjini Kampala Uganda mwezi Novemba mwaka jana, uliweka bayana kwamba ni katika mkutano huuu wa Arusha, ambapo tarehe ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki itakapotangazwa.
Lakini wadadisi wanasema kuwa msukosuko wa kiuchumi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe huenda ikawa sababu ya taifa hilo kunyimwa uanachama wa jumuiya hiyo. Hii ni baada ya machafuko ya wenyewe kwa
wenyewe kuzuka, na kusambaratisha nchi hiyo kisiasa na kiuchumi.
Maswala mengine yatakayojadiliwa ni ripoti ya mawaziri, mikakati ya kifedha katika kuiendesha jumuiya hiyo na mbinu za nchi wanachama kuendelea kupeana taarifa za kijasusi, katika juhudi za kupambana na tishio la ugaidi.
CHANZO BBC
Post a Comment