Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kuhusu Ajali ya Ndege ya JWTZ aina ya Helikopta katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyokuwa imewabeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dr. Ghalib Bilal na ujumbe wake ambao ni Waziri wa Ujenzi; Mhe. Dr. John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadick na amishina Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Kamishina Suleiman Kova.

 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa  vyombo vya habari na wananchi wote kwa ujumla kuwa jana tarehe 13 April 2014 mnamo saa tatu na nusu asubuhi (3:30 Hrs), kumetokea ajali ya Ndege ya JWTZ aina ya Helikopta katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere ( upande wa Jeshi). Helikopta hiyo ilipata ajali ilipokuwa katika hatua ya kuanza kuruka.
Helikopta hiyo ilikuwa imewabeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dr. Ghalib Bilal na ujumbe wake ambao ni Waziri wa Ujenzi; Mhe. Dr. John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadick na kamishina Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  Kamishina Suleiman Kova. 

Aidha, Wengine waliokuwemo ni Dr. Mnzava, Msaidizi wa Makamu wa Rais, Msaidizi wa Kamanda Kova na waandishi wa habari watatu.  

Ujumbe wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa  katika safari ya kuzungukia maeneo yaliyo athirika na mafuriko  katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kufuatia mvua kubwa iliyoanza kunyesha kuanzia tarehe 11 April hadi sasa.

Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake hawakupata majeraha katika ajali hiyo. Aidha, rubani na wasaidizi wake pia wametoka salama. 
Uchunguzi wa ajali  umeanza mara moja kwa ajili ya kubaini chanzo cha ajali hiyo. 

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0754270136

Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa  vyombo vya habari na wananchi wote kwa ujumla kuwa leo tarehe 13 April 2014 mnamo saa tatu na nusu asubuhi (3:30 Hrs), kumetokea ajali ya Ndege ya JWTZ aina ya Helikopta katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere ( upande wa Jeshi). Helikopta hiyo ilipata ajali ilipokuwa katika hatua ya kuanza kuruka.

Helikopta hiyo ilikuwa imewabeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dr. Ghalib Bilal na ujumbe wake ambao ni Waziri wa Ujenzi; Mhe. Dr. John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadick na amishina Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  Kamishina Suleiman Kova. 

Aidha, Wengine waliokuwemo ni Dr. Mnzava, Msaidizi wa Makamu wa Rais, Msaidizi wa Kamanda Kova na waandishi wa habari watatu.   

Ujumbe wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa  katika safari ya kuzungukia maeneo yaliyo athirika na mafuriko  katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kufuatia mvua kubwa iliyoanza kunyesha kuanzia tarehe 11 April hadi sasa.

Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake hawakupata majeraha katika ajali hiyo. Aidha, rubani na wasaidizi wake pia wametoka salama. 
Uchunguzi wa ajali  umeanza mara moja kwa ajili ya kubaini chanzo cha ajali hiyo. 

Imetolewa na 
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203,
 Simu: 0754270136
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top