Mmoja wa tembo waliouawa na majangili. |
Vitendo
vya ujangili vimepungua kwa asilimia 58 huku idadi ya meno ya tembo
yanayokamatwa, ikiwa imeongezeka, kutokana na kukamatwa meno
yaliyowindwa siku za nyuma.
Hayo yalisemwa jijini hapa jana na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Paul Sarakikya.
Alisema
hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya
habari, juu ya hali ya ujangili katika kipindi cha Januari hadi Machi
mwaka huu.
Alisema
katika kipindi hicho, siku za doria za kukabili ujangili zilikuwa
30,372 zilifanyika ndani na nje ya hifadhi za taifa na mapori ya akiba
nchini.
Alisema
katika kipindi husika, mizoga ya tembo 39 ilionekana ndani na nje ya
hifadhi za taifa na mapori ya akiba. Pia meno ya tembo mazima 171 na
vipande 22 vya meno ya tembo ghafi, vipande 302 vya meno ya tembo
yaliyochakatwa yenye jumla ya kilo 662.62, yalikamatwa, yakitokana na
vitendo vya ujangili.
Aidha
ng'ombe 2,663, msumeno na mbao 745 zilikamatwa. Jumla ya kesi 124 zenye
watuhumiwa 544 waliojihusisha na vitendo vya ujangili, zilifunguliwa
kwenye mahakama mbalimbali nchini.
Kesi
38 kati ya hizo zenye watuhumiwa 113, zinaendelea mahakamani na kesi 62
zenye jumla ya watuhumiwa 85 ziliishia kwa watuhumiwa kulipa faini ya
Sh 25,510,000.
Post a Comment