Mkurugenzi
wa Shirika la KIVULINI Bw Ramadhan Masele akifunga ziara ya kimafunzo
ya siku tatu kwa mbele ya washiriki wa ziara hiyo (hawapo pichani), Bw
Masele alitoa shukrani kwa maafisa toka mashirika matano ya mikoa ya
kanda ya ziwa pamoja na maafisa toka Mfuko wa Msaada wa kisheria (LSF)
na Foundation for Civil Society kwa ziara hiyo ya mafunzo.
|
Maafisa
Miradi pamoja na Maafisa Wakaguzi na Tathmini Miradi toka mashirika
matano ya Kiraia yanayopata ruzuku kutoka Mfuko wa Msaada wa Kisheria
(LSF) Tanzania, yamemaliza ziara ya kimafunzo ya siku tatu katika
Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na wasichana Tanzania, KIVULINI la
jijini Mwanza, ziara iliyolenga kujifunza na kuboresha
ufanyaji kazi wa mashirika hayo kupitia Miradi mbalimbali inayoendeshwa na KIVULINI.
ufanyaji kazi wa mashirika hayo kupitia Miradi mbalimbali inayoendeshwa na KIVULINI.
Mashirika
hayo matano toka mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mara, na Tabora yalianza
mafunzo hayo Jumatatu ya tarehe 28 Aprili, 2014 na kumaliza mafunzo hayo
tarehe 30 Aprili, 2014 kwa kutembelea Wasaidizi wa Kisheria wanaofanya
kazi ya kutoa elimu na ushauri wa kisheria katika vijiji mbalimbali vya
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba chini ya shirika
la KIVULINI kupitia mradi wa Msaada wa Kisheria unaofadhiliwa na LSF.
la KIVULINI kupitia mradi wa Msaada wa Kisheria unaofadhiliwa na LSF.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa Ziara hiyo Mkurugenzi wa Shirika la
KIVULINI Bw. Ramadhan Masele aliwashukuru maafisa wote toka mikoa hiyo
mitano ya kanda ya ziwa kwa kuhudhuria
mafunzo hayo lakini pia aliwashukuru Mfuko wa Msaada wa Kisheria kwa heshimawaliyowapa KIVULINI kuwa kituo cha mafunzo kwa asasi nyengine.
mafunzo hayo lakini pia aliwashukuru Mfuko wa Msaada wa Kisheria kwa heshimawaliyowapa KIVULINI kuwa kituo cha mafunzo kwa asasi nyengine.
“Ziara
hii imetoa hamasa nzuri hasa kwa upande wa kimahusiano baina ya Asasi
zinazotekeleza mradi wa msaada wa kisheria kwa kanda ya ziwa, pia uzoefu
tuliobadilishana kwa siku zote tatu za mafunzo naamini utaenda
kuimarisha utendaji kazi wa asasi zetu na kuinua hali ya maisha
ya Watanzania kupitia sisi” alisema Mkurugenzi wa KIVULINI Bw Ramadhan Masele.
ya Watanzania kupitia sisi” alisema Mkurugenzi wa KIVULINI Bw Ramadhan Masele.
“Lakini
pia tuwashukuru wadau wetu wakubwa katika mradii huu wa msaada wa
kisheria, LSF, kwa ubunifu waliouleta wa kutuwezesha kukutana pamoja na
kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi, na hivyo hivyo shukrani zetu
ziende kwa Foundation for Civil Society kwa kushirkiana
na SLF kuwa pamoja nasi, tunaomba huu uwe ni mwanzo tu na usiwe mwisho” alimalizia Bw Masele
na SLF kuwa pamoja nasi, tunaomba huu uwe ni mwanzo tu na usiwe mwisho” alimalizia Bw Masele
Ziara
hiyo imeratibiwa na LSF kwa kushirikiana na Foundation For Civil Society
kutoa hamasa na kuinua utendaji kazi wa Asasi za Kiraia nchini katika
kuhakikisha asasi hizo zinatoa matokeo bora katika mradi wa Msaada wa
kisheria.
Mashirika
yaliyohudhuria ziara hiyo ya Kimafunzo ni Jamii Salama Development
Volunteers (JSDV) toka Tabora, Centre for Widows and Children Assistance
(CWCA) la mkoani Mara, Mama’s Hope Organization for Legal Aid (MHOLA),
Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESHI), Sheria na Haki za Binadamu (SHEHABITA) la mkoani Mara.
Post a Comment