MKE
wa Rais, Mama Salma Kikwete, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, zinazotarajia kufanyika Mei
5, jijini Dar es Salaam.
Chama
cha Wakunga Tanzania (TAMA) kitaadhimisha siku ya Wakunga Duniani
(International Day of Midwives hapa nchini kwa siku mbili kuanzia tarehe
4hadi 5/2015.
Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa duniani kote tarehe tano mwezi wa tano ya kila mwaka.
Madhumuni
ya Maadhimisho hayo ni kuhamasisha Wadau mbalimbali pamoja na Jamii
kwa ujumla kuhusu umuhimu wa wakunga na shughuli wanazozifanya katika
kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo
vya watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano.
Kauli
Mbiu ya Mwaka huu (2014) ni “Wakunga Wataalam Wanahitajika Duniani kwa
wingi sasa kuliko siku zote.” (The World Needs Midwives Today Than Ever)
Hii
inalenga katika kuhakikisha kuwa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto
zinatolewa na Wakunga wenye utalaam kwa kufuata miongozo na viwango
vilivyowekwa ili kuchangia katika kufikia Malengo ya Maendeleo ya
Milenia namba 3,4, 5 na 6.
Tanzania
ni mmojawapo ya nchi zenye uhaba wa watao huduma wenye ujuzi
hususani Wakunga katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya ambako
ndiko wakinana mama wengi wanapata huduma ya wakiwa wajawazito,
kujifungua na baada ya kujifungua.
TANZANIA MIDWIVES ASSOCIATION (TAMA)
Address: HQ Dar Es Salaam
P.O. Box 65524 Dar Es Salaam Tanzania E-Mail: seolesh@yahoo.com
Katika kuadhimisha siku hiyo, Wakunga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watafanya shughili tatu ambazo ni:
1.
Kongamano la kisayansi kwa siku moja tarehe 4/5/2014 ambapo
watajadili mada na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakunga.
Mahali
: Hospitali ya Taifa ya Muhimhili Jengo la New OPD Chumba
no 60, linaloangaliana na Wadi ya Wazazi
Mgeni Rasmi: Mheshimiwa Dkt. Seif S Rashidi (MB) Waziri wa Afya na Ustawi Wa Jamii
2
Kutoa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika viwanja vya Mnazimmoja
kwa akina mama, watoto , vijana na wanaume kwa siku mbili 4/hadi 5/2014.
Huduma zitakazotolewa ni:
* Uzazi wa mpango,
* Chanjo kwa watoto
* Ushauri na upimaji wa hiari wa virus vya UKIMWI,
* Uchunguzi wa saratani ya matiti na kizazi kwa akina mama
* Utoaji wa hiari wa damu.
* Elimu na ushauri kuhusu hudma ya Afya ya Uzazi na Mtoto
* Wanaume watapata sindano ya Pepopunda ( tetanus)
Huduma zitakazotolewa ni bure hakuna malipo.
3
Kufanya mandamano kutoka makao makuu ya Wizara ya Afya hadi Viwanja
vya Mnazimmoja siku ya kilele tarehe 5/5/2014. Maandamano yataongozwa na
Brass band ya JKT Mgulani.
Mgeni Rasmi ni: Mheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mke wa Mh. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa heshima na taadhima Chama kinaomba vyombo vya habari kutusaidia kutoa taarifa kwa Wananchi.
Tunatanguliza shukurani zetu.
Dr Sebalda Leshabari KATIBU MKUU TAMA
Post a Comment