MJAMZITO
Agatha Isack (19) amekufa kwa kipigo kutoka kwa mumewe akisaidiwa na
mwanamke anayeaminika kuwa hawara yake, akimtuhumu kuwa mvivu wa kulima
shambani.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha kifo
hicho na kuongeza kuwa mama huyo mjamzito ambaye ni mkazi wa kijiji cha
Manga, Kata ya Kasokola wilayani Mlele alifikwa na umauti akikimbizwa
katika zahanati kijijini hapo kwa matibabu na mumewe huyo Vitus Mlengo
(23).
Akielezea
mkasa huo unaodaiwa kutokea juzi saa sita mchana nyumbani kwa wanandoa
hao kijijini humo, Kamanda Kidavashari alisema awali baada ya kipigo
mwanamke huyo alikwenda katika zahanati iliyopo kijijini humo kwa
uchunguzi zaidi na matibabu.
Kabla
ya kufika hospitalini alikwenda kwa mama yake mdogo aitwae Anastazia
Charles na kumsimulia jinsi alivyopigwa na mumewe akishirikiana na
Faustina Matheo (31) ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
Mlengo.
“Baada
ya kutibiwa Agatha alipitia nyumbani kwa bibi yake kijijini humo na
kumweleza jinsi alivyopigwa na mumewe pia alimfahamisha bibi yake kuwa
mumewe alimuonya asirudi nyumbani bila mboga hivyo bibi yake huyo
alimpatia mboga naye akarejea kwake,“ alibainisha Kamanda Kidavashari.
Inadaiwa
alipofika nyumbani kwa mumewe, Mlengo alimfukuza ndipo alirudi kwa
bibi yake na kulazimika kulala huko hadi asubuhi alipofuatana na bibi
yake ndipo mumewe akampokea.
Kidavashari
alifafanua kuwa juzi, saa mbili usiku Agatha alishindwa kula chakula
alichokipika mwenyewe ndipo mumewe alipoona hali yake imebadilika ndipo
alilazimika kuomba msaada wa pikipiki kwa rafiki yake aitwae Alfred
Kasonso na kumkimbiza katika zahanati kijijini humo kwa matibabu.
Kamanda alithibitisha kuwa mume wa marehemu huyo na Faustina wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
SOURCE: HABARI LEO
Post a Comment