Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
MOYO unauma! Baada ya
kutukanwa matusi ya nguoni kwenye mitandao ya kijamii na blogs, kwa
mara ya kwanza staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
amefunguka na kudai kwamba amechoka kutukanwa kila kukicha lakini pamoja
na hayo yote hatingishiki kwa lolote.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wolper alisema kuwa ni kweli amechoka lakini anawaachia nafasi watu wanaomchafua kwenye mitandao na hatishiki kwa lolote kwani maneno yao siyo ya kweli na kamwe hatamtangaza mpenzi wake kama ilivyokuwa zamani.
“Watukane sana, waseme mimi ni mwanaume lakini mimi ninatambua ninachokifanya, wakichoka wataacha. Kamwe sipo tayari kumweka mwanaume wangu kwenye vyombo vya habari, unajua kwenye mitandao kuna uchonganishi mwingi sana na mtu usipokuwa makini utajikuta ukimchukia mtu bila sababu kutokana na watu kuwa na mitazamo mbalimbali,” alisema Wolper.
Post a Comment