Sasa
ni dhahiri kwamba kuna msuguano wa wazi kati ya mihimili miwili ya
dola, Bunge na Serikali, kuhusiana na hatua ya Serikali kuchelewa
kutekeleza maazimio ya Bunge.
Msuguano
huo umeshika kasi wiki hii baada ya Serikali kuwarudisha kwenye
nyadhifa zao vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao hivi
karibuni waliondolewa na Waziri Lazaro Nyalandu, huku wabunge wakiapa
kuibana Serikali kuwang’oa viongozi hao.
Vigogo
hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa
na Mkurugenzi Msaidizi, Jaffar Kidegesho kwa madai ya kutowajibika
ipasavyo katika vita dhidi ya ujangili nchini.
Mbali
na sababu hiyo, lakini Nyalandu alikaririwa akisema alichukua uamuzi
huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mazimio 16 ya Bunge, yaliyotolewa
baada ya taarifa ya Operesheni Tokomeza Ujangili.
Post a Comment