Ikiwa ni mwezi mmoja tangu mlinzi wa kampuni ya K.K.security mjini Geita kuchinjwa hadi kufa na
mwili wake kutupwa kwenye mgahawa chini ya meza katika eneo la Mbugani
katika Kata ya Kalangalala mkoani hapa, mlinzi mwingine ameuawa kwa
kuchinjwa usiku wa kuamkia leo mjini hapa.
Tukio
hilo limetokea usiku wa wa kuamkia leo katika mtaa wa Shilabela ambapo
mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina la Juma Sunguta(48) anayeishi mtaa wa
Moringe amechinjwa na kuuawa wakati akiwa katika eneo lake la kazi
analolinda lililoko shilabela .
Imeelezwa kuwa mlinzi huyo ameuawa lakini wauaji hao hawakuchukua kitu chochote zaidi ya kumchinja na kuondoka.
Baadhi
ya watu wa eneo hilo waliioongea na mwandishi wa habari hizi baada ya
kufika kwenye eneo la tukio wamedai kuwa huenda ni chuki za kulipizana
visasi kwa sababu hapo kazini alikuwa anafanya kazi vizuri.
Afisa mtendaji wa kata ya Kalangalala Hussen Hamadi aliyefika kwenye
eneo la tukio amesema kuwa yeye amepigiwa simu asubuhi kuwepo kwa tukio
hili na alipoenda akakuta marehemu ametupwa nje ya maduka huku shingo
ikiwa imechinjwa .
Aidha Hamad ameongeza kuwa hali hiyo inasikitisha katika kata yake
kwani hivi karibuni mlinzi mwingine naye aliuawa eneo la mbugani kwa
hiyo kuna kila sababu ya kutafuta chanzo cha matukio hayo.
Baadhi
ya wakazi waliokuwa katika eneo hilo ambapo ni eneo la maduka
alipokuwa analinda marehemu wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa
matukio ya mauaji yamekuwa mengi na hivyo kuishi kwa wasiwasi.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani hapa kamishina msaidizi Joseph Konyo
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi wa tukio hilo
unaendelea ili kubaini waliofanya unyama huo na kisha wafikishwe kwenye
vyombo vya sheria.
Na Valence Robert Geita.
Post a Comment