Waethiopia
55 wamekamatwa na wanakijiji cha Chekereni Pabliki kilichopo Himo,
Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa wamejificha kichakani na mkazi
mmoja wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba watu hao walikamatwa ...
“Wanakijiji
walitoa taarifa polisi baada ya kuwaona watu hao, na sisi tulifika mara
moja kuwakamata wakiwa na mwenyeji wao,” alisema Kamanda Boaz.
Aliongeza: “Kwa sasa hatuwezi kumtaja jina wenyeji wa watu hao kwa vile bado tunaendelea na uchunguzi zaidi.”
Kwa
mujibu wa Kamanda Boaz, watu hao baada ya kuhojiwa walidai kuwa walikuwa
njiani kwenda nchini Afrika Kusini kupitia Tanzania.
Alisema
uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika wengine zaidi wa mtandao wa
kusafirisha binadamu kabla ya kufikishwa mahakamani.
Aliwataka
wananchi waishio mipakani kuendelea kuwa walinzi na kutoa taarifa
polisi pindi wanapowaona watu wanaowatilia shaka katika maeneo yao.
Post a Comment