Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MANGWEA JUNI 28, SAMAKI SAMAKI MOROGORO

Px 1Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’,  Kareeem Omary ‘KO’  (kushoto) akiwa na familia ya marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ Mama mzazi wa Mangwea (Katikati) na  kaka wa Mangwea, Keneth Mangwea  (kulia).
Albert Mangwair
Px2Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’,  Kareeem Omary ‘KO’ .
Px3
Bana ya Love Concert
px4Taswira ya Nyumbani kwa Mama Mangwea kwa sasa.
Albert MangwairMangwea enzi za uhai  wake
..Mastaa kibao kujumuika katika ‘LOVE CONCERT’
..Afande Selle, Belle 9, Samir na wengineo –Moro
P-Funky, Mswaki, Chemba Squad kutikisa 
Na Andrew Chale
MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha  marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ ,  litakalofanyika ndani ya ukumbi wa  Nyumbani Park (Samaki  samaki Spot) , Kihonda Morogoro mjini Juni 28.
Akizungumza na mtando huu , Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo,  Kareeem Omary ‘KO’  alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert – Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.
Kareem, aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani litakuwa la kipekee na la aina yake  ambalo pia litatoa fursa kwa wakazi hao pia mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao watauzulia. 
“Nawaomba wadau kujitokeza kuonesha  upendo  wa pamoja. Kumbukumbu  kwa mpendwa wetu kama ilivyo utamaduni wetu.” alisema Kareem.
Na kuongeza kuwa, siku hiyo   Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa  pamoja na mama mzazi wa Mangwea  kama kumbukumbu.
Kareem aliwataja wasanii watakaotoa burundani, ni pamoja  na kutoka kwa kundi la Wanachemba ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair,  JSqueezer, P Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9,  Samir, Zombie, President  Mirrow,  Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika siku hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu, Kareem alisema kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada mbili maalum ikiwemo ya  Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha, Kareem alisema katika tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya jioni ya saa 10 hadi saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani ikiwemo ya kuimba na nyinginezo  na baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi majogoo wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’  alifariki  dunia akiwa  nchini Afrika kusini, alijizolea umaarufu kwa nyimbo kama Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi alizowahi shirikishwa na wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Professa Jay, Nuru, TID, Chidi Benz  na wengine wengi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top