Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LUGOLA AWASHIA MOTO MPYAAA WA MUSWADA WA VAT


Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola amesema iwapo Muswada wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), hautapelekwa bungeni, atakusanya saini za wabunge ili kumwondoa madarakani Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Lugola aliyasema hayo jana alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika ni lini muswada huo unaolenga kufuta misamaha ya kodi utaletwa bungeni.
Alisema amepata taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wake wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya
Mitaa (Laac), Rajab Mborouk Mohamed ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi kuwa kamati hiyo iliiagiza Serikali kuwasilisha haraka Muswada wa VAT.
Alisema lengo la kutaka muswada huo uletwe bungeni ni kupitia na kufuta misamaha yote ya kodi isiyo na tija.
Alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2012/2013 inaonyesha kuwa kuna misamaha ya kodi ya Sh1.5 trilioni nchini.
"Bajeti yetu ya mwaka jana inaonekana ina upungufu wa Sh1.5 trilioni na kusingekuwa na misamaha ya kodi mwaka jana tusingekuwa na upungufu huo," alisema.(Martha Magessa)
"Wabunge tumekuwa tukiilazimisha Serikali iongeze fedha. Wabunge ndiyo waliomchagua Spika na Spika ameonyesha kuipendelea Serikali ilhali wananchi wanashindwa kupata maendeleo," alisema.
Alihoji ni lini muswada huo utaletwa bungeni kwa sababu karibu Bunge la Bajeti linaelekea ukingoni.
"Haya mambo ya wabunge kutishwatishwa kwamba tukikataa Bajeti ya Serikali Bunge litavunjwa. Mimi niko tayari Bunge livunjwe nirudi Mwibara nikalime na kuvua dagaa," alisema.
Alisema kama muswada huo hautaletwa katika Bunge la Bajeti atakuwa mbunge wa kwanza kuleta hoja ya kumtaka spika afukuzwe kwenye kiti hicho kwa sababu anaibeba Serikali.
Alipoulizwa baadaye jana jioni sababu ya kumng'ang'ania Spika, Lugola alisema: "Ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ambayo hupanga ratiba. Ukitazama ratiba ya mkutano huu, hakuna mahali panapoonyesha Serikali italeta muswada huo wa VAT badala yake, Serikali inasema tu kwa mdomo na yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi," alisema Lugola.
Akijibu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Serikali ndiyo iliyoomba kuleta Muswada wa VAT katika Bunge hili bajeti... "Hana sababu ya kumsingizia Spika kuibeba Serikali.
CHANZO:MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top